IRINGA


The name Iringa, comes from the word Lilinga which in Kihehe language means the Fort.The Wahehe is the tribe that owned this area had put a fort here so as to monitor enemies before they would reach the chief's palace in Kalenga. The Germans also came to build their fort on top of this hill, after they managed to conquer the Wahehe in the second battle between them.In he first encounter the Germans were truly beaten, their commander Von Zelewiski was killed and a few of his men were spared and sent back to warn their masters never to come back to the Wahehe land. Zelewiski's grave still exists at Lugalo a few kilometers from Iringa town. This blog is about this great town Iringa. And I was lucky to have been born here.
Welcome

Tuesday, October 25, 2016

MBUNGE VENANCE MWAMOTO AGAWA VIFAA VYA MICHEZO KATIKA JIMBO LA KILOLO


Na Fredy Mgunda, Iringa.
Mbunge wa Jimbo la Kilolo Venance Mwamoto amegawa vifaa mbalimbali vya michezo kama alivyowahidi kwa Vijana na timu  za Jimbo hilo kwa lengo la kukuza vipaji vya wanamichezo na kuwandeleza ili wawe wachezaji bora hapo baadae.

Mwamoto ametekeleza ahadi hiyo katika Vijiji mbalimbali vinavyounganisha Jimbo hilo la Kilolo katika ziara yake inayoendelea ya kuwashukuru wananchi wake kwa kuweza kumchagua kwa kura nyingi na kwenda kuwaakilisha Bungeni.

Akielezea wakati wa kutoa vifaa hivyo vya Michezo, Mwamoto amebainisha kuwa, vifaa hivyo anavitoa ni  kutokana na ahadi yake  yeye kama Mbunge aliiahidi kwa Vijana hao kuwapatia vifaa hivyo huku  baadhi yao pamoja na timu zilimuomba vifaa hivyo ambapo sasa anafanya kutekeleza.

“Niliahidi kuleta vifaa vya Michezo kwa kila Kata, na leo hii natimiza ahadi yangu kwenu.” Alieleza Mwamoto.
Mwamoto ameongeza kwa kusema ameamua kutoa vifaa hivyo kwa lengo la kusaidia Serikali katika juhudi za kuinua michezo lakini pia ni sehemu ya kazi zake kama Mbunge.
“Mimi nimecheza mpira kwa mafanikio kwa hiyo najua kuwa michezo ni ajira rasmi hivyo mtu kama unakipaji kitumie kipaji chako vizuri”. Mwamoto pia amesema kuwa michezo, licha ya kujenga utimamu wa mwili, lakini pia ni ajira huku akitoa mfano Kwa Mbwana Samatta alivyofanikiwa.
“Leo nimetoa mipira na jezi hizi kwa timu za Bomalang’ombe na vijiji vya jirani kwa timu zote za wanaume na wanawake kwa lengo la kuendeleza vipaji vyenu”alisema Mwamoto
Aidha, amewataka Vijana hao kuwa na tabia ya kufanya mazoezi ya mara kwa mara kwani yatawasaidia kufanya vizuri katika mpira wa miguu na pia mazoezi ni afya.

No comments:

Post a Comment