IRINGA


The name Iringa, comes from the word Lilinga which in Kihehe language means the Fort.The Wahehe is the tribe that owned this area had put a fort here so as to monitor enemies before they would reach the chief's palace in Kalenga. The Germans also came to build their fort on top of this hill, after they managed to conquer the Wahehe in the second battle between them.In he first encounter the Germans were truly beaten, their commander Von Zelewiski was killed and a few of his men were spared and sent back to warn their masters never to come back to the Wahehe land. Zelewiski's grave still exists at Lugalo a few kilometers from Iringa town. This blog is about this great town Iringa. And I was lucky to have been born here.
Welcome

Monday, December 26, 2016

MBUNGE RITTA KABATI KUKARABATI SHULE YA MSINGI AZIMIO SIKU YA IJUMAA TAREHE 23 MWEZI WA KUMI NA MBILI.

Mwenyekiti wa  Chama Cha Mapinduzi (CCM), wilaya  ya Iringa Abeid Kiponza, na Mbunge wa Viti Maalumu mkoani Iringa  kupitia CCM, Ritta Kabati na Mkuu wa Wilaya ya Iringa Richard Kasesela wakiwa katika moja ya madarasa ya shule ya msingi Azimio wakati wa kujadili jinsi gani ya kutatua changamoto za shule hiyo
Mbunge wa viti maalumu mkoani iringa  kupitia chama cha mapinduzi (CCM) Ritta Kabati akikagua miundombinu ya shule ya msingi Azimio sambamba na wananchi na viongozi wa shule hiyo.

Hili ni moja kati ya madarasa ya shule ya msingi Azimio ambalo lipo taabani kabisa na likiwa linakaribia kuanguka kutokana na kuwa na nyufa nyingi ambazo ni kubwa sana

Hili ni moja kati ya  madarasa ya shule ya msingi Azimio ambao linaonekana afadhari kidogo na kuwashawishi viongozi mbalimbali kuketi na kujadili maswala ya kutatua changamoto za shule hiyo ambapo madarasa mengine yapo taabani kuliko hili.

Mbunge wa viti maalum mkoani Iringa Ritta Kabati ameanza kazi ya  kukarabati shule ya msingi ya Azimio iliyopo Manispaa ya Iringa kutokana na uchakavu wa majengo ya shule hiyo.

Akizungumza wakati wa ukaguzi wa miundombinu ya shule hiyo Mbunge Kabati alisema ni aibu kwa shule kongwe kama hiyo  kuwa miundombinu mibovu kama hiii.

Kabati aliongeza kuwa shule hiyo imeharibika mno hivyo inahitaji msaada wa haraka kuikarabati kwa kuwa wanafunzi wanasoma katika mazingira magumu.

“Hii shule imeanza sawa na siku niliyozaliwa mimi lakini ukiiangalia imechakaa na imechoka hivyo sina budi kuanza kuikarabati shule hii kwa kuwa ni aibu kwangu haiwezakani shule ikawa ndani ya Manispaa ya Iringa kisha ikawa katika hali mbaya hivi” alisema Kabati.

Aidha Kabati alisema kuwa hadi kufikia siku ya Ijumaa ya tarehe 23 mwezi Desemba 2016, atahakikisha anakarabati shule yote ili iwe  katika ubora unaotakiwa kama shule nyingine zilizopo manispaa ya Iringa.

“Tuna shule bora sana hapa Manispaa ya Iringa lakini hii ya Azimio imekuwa katika hali mbaya sana ni jukumu langu kama mbunge wa mkoa wa Iringa kutatua changamoto mbalimbali zinazoukabili mkoa wangu” alisema Kabati

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Iringa Richard Kasesela aliunga mkono mawazo ya Mbunge, na kuomba ushirikiano wa wadau mbalimbali.

Naye mkuu wa shule ya hiyo, Willfrid Chotipembe alimshukuru Mbunge wa viti maalum Ritta Kabati pamoja na Mkuu wa Wilaya kwa kufika shuleni hapo na kuahidi kutatua changamoto zinazoikabili shule hiyo.
Habari hii imeletwa na   Fredy Mgunda, Iringa

No comments:

Post a Comment