IRINGA


The name Iringa, comes from the word Lilinga which in Kihehe language means the Fort.The Wahehe is the tribe that owned this area had put a fort here so as to monitor enemies before they would reach the chief's palace in Kalenga. The Germans also came to build their fort on top of this hill, after they managed to conquer the Wahehe in the second battle between them.In he first encounter the Germans were truly beaten, their commander Von Zelewiski was killed and a few of his men were spared and sent back to warn their masters never to come back to the Wahehe land. Zelewiski's grave still exists at Lugalo a few kilometers from Iringa town. This blog is about this great town Iringa. And I was lucky to have been born here.
Welcome

Monday, March 13, 2017

KATIBU TAWALA IRINGA JOSEPH CHITINKA CHEZENI MPIRA ACHENI KUKAA VIJIWENI

Katibu Tawala wilaya ya Iringa, Joseph Chitinka akiwasalimia wachezaji wa timu ya Waandishi wa habari mkoa wa Iringa (IMFC) kabla ya mchezo kati yao dhidi ya timu ya kijiji cha Mangalali uliochezwa katika uwanja wa Kalenga kwenye mashindano ya Mbuzi Cup. Katibu tawala wilaya ya Iringa Joseph Chitinka akiwa katika picha ya pamoja na  wachezaji wa timu ya Waandishi wa habari mkoa wa Iringa (IMFC) kabla ya mchezo kati yao dhidi ya timu ya kijiji cha Mangalali uliochezwa katika uwanja wa Kalenga kwenye mashindano ya Mbuzi Cup.
 Katibu tawala wilaya ya Iringa Joseph Chitinka akiwa katika picha ya pamoja na  wachezaji wa timu ya kijiji cha Mangalali kabla ya mchezo kati yao dhidi ya timu ya Waandishi wa habari mkoa wa Iringa (IMFC) uliochezwa katika uwanja wa Kalenga kwenye mashindano ya Mbuzi Cup.
Na Fredy Mgunda,Iringa.

MASHINDANO ya kombe Mbuzi Cup yatafikia tamati tarehe 30 mwezi wa tatu kwa kuzikutanisha timu za Mkwawa Rangers na Waandishi wa habari mkoa wa Iringa na fainali hiyo itachezwa katika kijiji cha Kalenga kata ya Kalenga wilayani Iringa mkoani Iringa ikiwa lengo la kuinua vipaji wa wachezaji kata hiyo.

Akishudia mchezo wa nusu fainali kati ya timu ya Waandishi wa habari mkoa wa Iringa (IMFC) na timu ya kijiji cha Mangalali uliochezwa katika uwanja wa Kalenga, Katibu Tawala wilaya ya Iringa Joseph Chitinka ambaye alikuwa mgeni rasmi alisema ni wakati mzuri kwa sasa kuyageukia mashindano ya mchangani kwani yamesheheni vipaji vingi vitakavyosaidia kuendeleza mpira wa Tanzania wakati ambapo taifa likiendelea kupata matokeo yasiyoridhishwa kwenye soka kwa sasa,

"Mashindano haya ni muhimu sana kwa wakati huu kwani yatasaidia kuinua vipaji vya vijana wetu na kuweza kupata timu bora ya taifa hivyo nidhamu ni muhimu wakati wa michezo hiyo" alisema Chitinka

Aidha Chitinka aliongeza kwa kusema kuwa mpira wa miguu umekuwa na faida kwa wachezaji kwani wanaweza kujitengezea vyanzo vya ajira kama Mbwana Samatta na wachezaji wengine wanalipwa vizuri hapa nchini hata nje ya nchi.

 “Mwaka huu tumekuja na wataalamu wanachagua vipaji maalumu kwa ajili ya kujiunga na timu mbalimbali na lengo likiwa ni kuhakikisha vipaji vyote vinaonekana na vinafika mbali kwa kuwa sasa mpira ni ajira.” alisema Chitinka
  
Mwenyekiti wa Kamati ya Mashindano hayo Obeid Msigwa aliwataka washiriki wa mashindano hayo kujituma ili ipatikane timu ya bora ambayo itakuwa ikiwakilisha katika mashindano ya mbalimbali.

“Soka imewapa ajira mamilioni ya wachezaji na viongozi ulimwenguni na wameweza kuishi maisha ya kifahari kutokana na mishahara wanayopata”, alisema Msigwa

Kwa upande wake mlezi wa mashindano hayo kamanda wa vijana wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wilaya Iringa Jackson Kiswaga alisema ataendelea kuwaunganisha vijana kupitia michezo na kusaidia kukuza mpira wa wilaya ya Iringa.

“Ilani ya Chama Cha Mapinduzi inatutaka mwenyeviti kote nchini kuhakikisha michezo inafanyika mara kwa mara na kuleta tija kwa taifa ili tuondokane kuwa kuwa vichwa vya wendawazimu”alisema Kiswaga.

Mashindano ya Mbuzi Cup ni miongoni mwa mashindano yanayolenga kuibua vipaji vya vijana vijijini ili kuwawezesha kupata nafasi ya kucheza katika vilabu vikubwa nchini.

Friday, March 3, 2017