MKWAFI MNYAKIDADA

Thursday, January 18, 2018

MHE BITEKO AMUAGIZA KAMISHNA WA MADINI KANDA YA KUSINI KUANZISHA OFISI YA MADINI WILAYANI RUANGWA

Naibu Waziri wa Wizara ya Madini Mhe Doto Mashaka Biteko akizungumza na wachimbaji wadogo kwenye mkutano wa hadhara katika kitongoji cha Namungo Kata ya Megembekenyela Wilaya ya Ruangwa wakati wa ziara yake ya kikazi mkoani Lindi, Leo 8 Januari 2018. Picha Zote Na Mathias Canal

REGISTRATION IS NOW OPEN FOR PUBLIC LECTURE ON KOREAN EXPERIENCE ON ECONOMIC TRANSFORMATIONFURSA YA SCHOLARSHIP KWA: SHULE ZA SEKONDARI, MAOMBI YATUMWE SASA KUSHIRIKI MAONYESHO YA SAYANSI YA YST 2018
 Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Profesa Simon Msanjila akikabidhi zawadi kwa Prosper Gasper na Erick Simon kutoka Shule ya Sekondari St. Jude's jijini Arusha baada ya kuibuka washindi wa jumla wa Mashindano ya Wanasayansi Chipukizi (YST) yaliyofanyika leo yaliyofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC) jijini Dar es Salaam.

MAGASETI ALHAMISI 18 JANUARI 2018


MSANII MBUNIFU TOKA IRINGA

RAIS MAGUFULI AMTEUA DR TITUS MWINUKA KUWA MKURUGENZI MTENDAJI WA TANESCOWednesday, January 17, 2018

WHAT IS TRUTH?

MWENYEKITI WA UVCCM KHERI D JAMES AKUTANA NA KUFANYA MAZUNGUMZO NA VIONGOZI MBALI MBALI WA UVCCM MKOA WA DAR ES SALAAM.


Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi Ndg.Kheri Denis James(MCC) akizungumza  kwa Msisistizo wakati wa kikao na Wajumbe wa kamati ya Utekelezaji ya mkoa wa dar esa salaam pamoja na Baraza kuu la Vijana Wilaya ya Kinondoni, kulia ni Kaimu Katibu mkuu wa UVCCM Taifa Shaka Hamdu Shaka na Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Dar Es Salaam Mussa Kilakala,Katika Ofisi ndogo ya Makao makuu ya UVCCM Upanga Dar es Salaam.

Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi Ndg.Kheri Denis James(MCC) akizungumza wakati wa kikao na Wajumbe wa kamati ya Utekelezaji ya mkoa wa dar esa salaam pamoja na Baraza kuu la Vijana Wilaya ya Kinondoni ,Katika Ofisi ndogo ya Makao makuu ya UVCCM Upanga Dar es Salaam.

Kaimu Katibu mkuu wa UVCCM Taifa Shaka Hamdu Shaka akizungumza wakati wa kikao na Wajumbe wa kamati ya Utekelezaji ya mkoa wa dar esa salaam pamoja na Baraza kuu la Vijana Wilaya ya Kinondoni ,Katika Ofisi ndogo ya Makao makuu ya UVCCM Upanga Dar es Salaam.

 Baadhi ya Wajumbe wakifuatilia kwa Umakini kikao hicho.

kikao kikiendelea.

Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi Ndg.Kheri Denis James(MCC) akizungumza  kwa Msisistizo wakati wa kikao cha Viongozi wa Seneti  Vyuo na Vyuo Vikuu Mkoa wa Dar es Salaam pamoja na Viongozi wa Matawi yote ya Vyuo na vyuo vikuu mkoa wa Dar es Salaam , kulia ni Kaimu Katibu mkuu wa UVCCM Taifa Shaka Hamdu Shaka na Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Dar Es Salaam Mussa Kilakala,Katika Ofisi ndogo ya Makao makuu ya UVCCM Upanga Dar es Salaam.

 Sehemu ya Wajumbe wa Vyuo na Vyuo Vikuu wakifurahia jambo(PICHA ZOTE NA FAHADI SIRAJI)
 ....................................................................................................................................................................


Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Cha Mapinduzi Ndugu Kheri Denis James (MCC) leo amekutana na kufanya mazungumzo na kamati ya Utekelezaji ya Mkoa wa Dar es Salaam pamoja na wajumbe wa Baraza la Vijana (UVCCM) Wilaya ya Kinondoni kuzungumzia maandalizi ya Uchaguzi wa marudio utakaofanyika tarehe 17 Februari, 2018.

Pamoja na mambo mengine Mwenyekiti amesisitiza kuwa  nguvu ya Vijana wa CCM itumike vizuri katika kuhakikisha CCM inashinda kwa kishindo Uchanguzi huo.  ''Suala la ushindi wa CCM katika uchaguzi huu wa marudio halina mjadala tutashinda kwa heshima, Amani na  demokrasia vijana wa CCM tumejipanga vyema kufanikisha hilo ngazi zote" Alisisitiza  Mwenyekiti Kheri

Wakati huo amekutana na kufanya mazungumzo na Viongozi wa Seneti ya Vyuo na Vyuo Vikuu Mkoa wa Dar es Salaam pamoja na Viongozi wa Matawi yote ya Vyuo na Vyuo Vikuu vilivyopo Mkoa wa Dar es Salaam. ''Tunatambua na kuthamini mchango wa Vijana wenzetu wote katika jamii mkiwemo ninyi wa Vyuo na Vyuo Vikuu tunawategemea sana hivyo tutaendelea kufanya kazi nanyi katika maeneo yote katika kutimiza wajibu wetu wa msingi” Alibainisha Mwenyekiti Kheir.
Mazungumzo hayo yamehudhuriwa na Kaimu Katibu Mkuu UVCCM Taifa Shaka Hamdu Shaka, Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Dar es Salaam Mussa Kilakala, Mwenyekiti wa Seneti Mkoa wa Dar es Salaam Asha Feruzi pamoja na Mjumbe wa Baraza kuu Taifa Alex Gwantwa.
 MICHANGO SHULE ZA SERIKALI MARUFUKU ASEMA RAIS

Rais Dkt.John Pombe Magufuli amepiga marufuku aina yoyote ya michango katika shule za serikali za msingi na sekondari. 

Akielezea hilo Rais alisema, ’Tumesema elimu bure, elimu bure haiwezi ikaja tena kwa mgongo mwingine ikawa elimu pesa. Tumeweka utaratibu kuanzia shule ya msingi mpaka sekondari kidato cha nne, hakuna kulipa ada yoyote. Nimewapa maelekezo kwamba kuanzia leo iwe ni marufuku na wakalisimamie hili. Mzazi sitaki kusikia akilalamika mwanae amerudishwa shule kwa sababu ya michango’. Rais aliendelea, ‘Na walimu wote wasishike mchango wowote toka kwa mwanafunzi, kama kuna mwananchi anataka kuchangia apeleke kwa mkurugenzi, mkurugenzi kama anataka kutengeneza madawati atatengeneza na kupeleka kwenye shule inayohusika. Siyo mwanafunzi ameenda shuleni akarudishwa kwa sababu hajatoa michango. Kwahiyo nimemweleza waziri na waziri mwenzake (Waziri wa TAMISEMI Mhe. Selemani Jafo na Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi Profesa Joyce Ndalichako)   kwa sababu ndio wanaoshughulikia elimu. Lakini kwa taarifa hii mkawaeleze wakuu wa mikoa, na wakurugenzi, nikisikia kuna shule katika wilaya fulani ambayo mtoto anarudishwa kwa sababu hajachangia michango huyo mkurugenzi hana kazi. Na hii waanze kutekeleza kuanzia leo. Maafisa elimu wote wakasimamie hili, wanalipwa kwa ajili ya kusimamia. Tunajua enrolment ya wanafunzi imeongezeka hizi ni challenge ambazo lazima tuzibebe sisi kama serikali lakini hii isiwe sasa ni demotivation nyingine ya kuwazuia watoto, sasa hivi watoto wameacha kwenda shule kutokana na michango hii inayotolewatolewa sasa waziri mkalisimamie hili’.

NYUMBA YA KATIBU WA UVCCM IRINGA MJINI YACHOMWA MOTO USIKU WA KUAMKIA LEOSehemu ya mali iliyoteketea

Mjumbe Wa Halmashauri kuu ya taifa Ccm Mnec Salim Asas akitoa salaam za pole

Mwathirika wa tukio akiwaonyesha viongozi wenzie, wanahabari, na wananchi  madhara aliyoyapata

Jana Jumanne kiasi cha saa tano usiku, kwa mujibu wa Alphonce Muyinga, alipokuwa amepumzika akasikia kioo cha chumba alichokuwa amelala kikivunjika na kitu kilitupwa ndani, baada ya hapo moto ukawaka. Moto huo umeunguza kila kitu kilichokuwa katika nyumba hiyo iliyopo maeneo ya Kihesa njiapanda ya Kwabeda . Kwa mujibu wa Kamanda wa zima moto James John, wao walipofika eneo hilo moto ulikuwa umeshika nyumba nzima hivyo walichojitahidi kufanya ni kuzuia moto usisambae nyumba za jirani, kamanda huyo amesema kutokana na maelezo ya Muyinga ambaye ni Katibu wa UVCCM Iringa mjini italazimika kuanza kufanya uchunguzi ili kujua waliohusika katika tukio hilo. Katibu Alphonce Muyinga anaamini kuwa kuchomewa nyumba huko ni kutokana na sababu za kisiasa

Comments system

Disqus Shortname

Comments System

blogger/disqus/facebook

Disqus Shortname