MKWAFI MNYAKIDADA

Thursday, December 29, 2016

JUST DON'T MISS THIS SHOW AT KING SOLOMON'S HALL NAMANGA DAR ES SALAAM

Utakosaje?Tiketi zinapatikana sasa EATERS POINT Namanga na Masaki. Tiketi za VIP Zimebaki chache. Pia tiketi zitauzwa mlangoni kuanzia saa mbili usiku. Njoo usikilize muziki tofauti na kucheza mpaka usiku mkali
You can't miss this.Tickets are available at EATERS POINT Namanga and Masaki. Limited VIP Tickets. Tickets will also be sold at the door from 8pm. Come and enjoy different varieties of music and dance tour heart out
JOHN KITIME &WAHENGA BAND

JOHN MHINA & THE TANZANITES

TAJ MBARAKA MWINSHEHE


MUSIC MAYDAY ARTISTS

Tuesday, December 27, 2016

AFTER XMASS IN PICTURESMBUNGE RITTA KABATI KUKARABATI SHULE YA MSINGI AZIMIO SIKU YA IJUMAA TAREHE 23 MWEZI WA KUMI NA MBILI.

Mwenyekiti wa  Chama Cha Mapinduzi (CCM), wilaya  ya Iringa Abeid Kiponza, na Mbunge wa Viti Maalumu mkoani Iringa  kupitia CCM, Ritta Kabati na Mkuu wa Wilaya ya Iringa Richard Kasesela wakiwa katika moja ya madarasa ya shule ya msingi Azimio wakati wa kujadili jinsi gani ya kutatua changamoto za shule hiyo
Mbunge wa viti maalumu mkoani iringa  kupitia chama cha mapinduzi (CCM) Ritta Kabati akikagua miundombinu ya shule ya msingi Azimio sambamba na wananchi na viongozi wa shule hiyo.

Hili ni moja kati ya madarasa ya shule ya msingi Azimio ambalo lipo taabani kabisa na likiwa linakaribia kuanguka kutokana na kuwa na nyufa nyingi ambazo ni kubwa sana

Hili ni moja kati ya  madarasa ya shule ya msingi Azimio ambao linaonekana afadhari kidogo na kuwashawishi viongozi mbalimbali kuketi na kujadili maswala ya kutatua changamoto za shule hiyo ambapo madarasa mengine yapo taabani kuliko hili.

Mbunge wa viti maalum mkoani Iringa Ritta Kabati ameanza kazi ya  kukarabati shule ya msingi ya Azimio iliyopo Manispaa ya Iringa kutokana na uchakavu wa majengo ya shule hiyo.

Akizungumza wakati wa ukaguzi wa miundombinu ya shule hiyo Mbunge Kabati alisema ni aibu kwa shule kongwe kama hiyo  kuwa miundombinu mibovu kama hiii.

Kabati aliongeza kuwa shule hiyo imeharibika mno hivyo inahitaji msaada wa haraka kuikarabati kwa kuwa wanafunzi wanasoma katika mazingira magumu.

“Hii shule imeanza sawa na siku niliyozaliwa mimi lakini ukiiangalia imechakaa na imechoka hivyo sina budi kuanza kuikarabati shule hii kwa kuwa ni aibu kwangu haiwezakani shule ikawa ndani ya Manispaa ya Iringa kisha ikawa katika hali mbaya hivi” alisema Kabati.

Aidha Kabati alisema kuwa hadi kufikia siku ya Ijumaa ya tarehe 23 mwezi Desemba 2016, atahakikisha anakarabati shule yote ili iwe  katika ubora unaotakiwa kama shule nyingine zilizopo manispaa ya Iringa.

“Tuna shule bora sana hapa Manispaa ya Iringa lakini hii ya Azimio imekuwa katika hali mbaya sana ni jukumu langu kama mbunge wa mkoa wa Iringa kutatua changamoto mbalimbali zinazoukabili mkoa wangu” alisema Kabati

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Iringa Richard Kasesela aliunga mkono mawazo ya Mbunge, na kuomba ushirikiano wa wadau mbalimbali.

Naye mkuu wa shule ya hiyo, Willfrid Chotipembe alimshukuru Mbunge wa viti maalum Ritta Kabati pamoja na Mkuu wa Wilaya kwa kufika shuleni hapo na kuahidi kutatua changamoto zinazoikabili shule hiyo.
Habari hii imeletwa na   Fredy Mgunda, Iringa

Tuesday, December 13, 2016

LETS REMEMBER PLACES IN IRINGA PART 1

Former Aga Khan Primary School

Former Aga Khan Secondary School


Former Iringa HotelTIGO YATOA MAPENDEKEZO YA KUOMBA KUORODHESHA HISA KATIKA SOKO LA HISAMwenyekiti wa bodi ya Wakurugenzi wa kampuni ya simu za mkononi ya Tigo balozi (mstaafu) Ami Mpungwe (katikati) akishirikiana na Mkurugenzi Mtendaji  wa kampuni hiyo, Diego Gutierrez wakikabidhi kabrasha lenye mapendekezo ya kuomba kuorodhesha hisa katika soko la hisa la Dar Es Salaam (DSE) kwa Afisa Mtendaji Mkuu wa soko hilo, Moremi Marwa.


Dar es Salaam – Desemba 8, 2016 –Kampuni ya Mtandao wa Simu za Mkononi ya MIC Tanzania Limited (Tigo) leo imetangaza rasmi kuwasilisha muhtasari  na maombi ya awali  katika Mamlaka ya Masoko ya Mitaji  na Dhamana (CMSA) na Soko la Hisa Dar es Salaam (DSE) kuhusiana na mapendekezo ya awali ya kuorodhesha hisa zake katika Soko la Hisa la Dar es Salaam.
Uuzwaji wa hisa hizo unatarajiwa kuanza mara baada ya CMSA na DSE kumaliza mchakato wa mapitio kulingana na masharti yanayohusu soko la hisa.
Akizungumza wakati wa uwasilishaji huo Mkurugenzi Mtendaji wa Tigo, Bwana Diego Gutierrez, alisema: “Tunayo furaha kutangazia umma kuhusu uwasilishaji wa muhtasari wetu  ili mchakato uanze rasmi na kwamba tutawapatia  wateja wetu, wafanyakazi wetu na Watanzania kwa ujumla  fursa ya kuwa wamiliki wa hisa ndani ya kampuni yetu.”
Mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi ya MIC Tanzania Limited, Balozi (Mstaafu) Ami Mpungwe aliongeza kuwa: “uwasilishaji huu ni hatua muhimu katika historia ya kampuni na kwamba utawapatia Watanzania wote fursa sawa ya kushiriki katika mtaji wa kampuni yetu katika siku za usoni. Tutafanya kazi pamoja na mamlaka za usimamizi kuhakikisha mchakato huu unafanyika ipasavyo.”


Friday, December 9, 2016

Comments system

Disqus Shortname

Comments System

blogger/disqus/facebook

Disqus Shortname