MKWAFI MNYAKIDADA

Friday, February 24, 2017

TPDC WATOA MAFUNZO KWA WAANDISHI WA HABARI WA MIKOA YA IRINGA,NJOMBE NA RUVUMA

Wanahabari mkoa  wa  Iringa  walioshiriki  warsha ya siku  moja ya gesi asilia  wakiwa katika picha ya pamoja na mkuu wa wilaya ya  Iringa Richard Kasesela wa  tatu  kutoka  kushoto na wawezeshaji wa  warsha hiyo  kutoka TPDC,warsha iliyofanyika  ukumbi wa  VETA  Iringa kwa  kushirikisha  wanahabari kutoka mkoa  wa  Njombe ,Ruvuma na wenyeji  Iringa.
 Wanahabari mkoa  wa  Njombe   walioshiriki  warsha ya siku  moja ya gesi asilia  wakiwa katika picha ya pamoja na mkuu wa wilaya ya  Iringa Richard Kasesela wa  tatu  kutoka  kushoto na wawezeshaji wa  warsha hiyo  kutoka TPDC,warsha iliyofanyika  ukumbi wa  VETA  Iringa kwa  kushirikisha  wanahabari kutoka mkoa  wa  Njombe ,Ruvuma na wenyeji  Iringa 

Wanahabari mkoa  wa  Ruvuma   walioshiriki  warsha ya siku  moja ya gesi asilia  wakiwa katika picha ya pamoja na mkuu wa wilaya ya  Iringa Richard Kasesela wa  tatu  kutoka  kushoto na wawezeshaji wa  warsha hiyo  kutoka TPDC,warsha iliyofanyika  ukumbi wa  VETA  Iringa kwa  kushirikisha  wanahabari kutoka mkoa  wa  Njombe ,Ruvuma na wenyeji  Iringa 
 Meneja mahusiano wa Shirika la Maendeleo ya Petroli na gesi Tanzania Maria Mselemu (TPDC)  akitoa  neno wakati wa utangulizi wa warsha hiyo kwa waandishi wa habari wa mikoa ya Iringa,Njombe na Ruvuma.

Na Fredy Mgunda,Iringa.
Mkuu wa Wilaya ya Iringa Mh. Richard Kasesela amelipongeza Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) kwa kuendesha mafunzo maalum kwa waandishi wa Habari wa Mikoa ya Arusha, Iringa,Ruvuma na Njombe  ameyasema hayo wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya siku moja ambayo yamefanyika mwezi wa pili tarehe ishirini na moja mwaka huu (21 / 02 /2017) katika ukumbi wa Chuo cha VETA mkoani Iringa.

“Ingawa mafunzo ni mafupi lakini napenda kulipongeza Shirika letu la Mafuta la Taifa kwa kuona umuhimu wa vyombo vya habari katika kupata uelewa mpana wa Sekta Ndogo ya Mafuta na Gesi ili waweze kuhabarisha na kuelimisha watanzania kwa ujumla ili watambue shughuli za shirika na faida zake haswa katika uchumi wa nchi”, alieleza Mkuu wa Wilaya.

Aidha Mh Kasesela amewaomba Waandishi wa Habari kuwa wazelendo katika kuisaidia Serikali kutekeleza miradi mbalimbali yenye maslahi mapana katika maendeleo ya nchi yetu.

‘’Waandishi Wahabari mnapaswa kuisaidia Serikali katika utekelezaji wa miradi mbalimbali yenye tija kwa uchumi wa Taifa, mfano katika vita ya kiuchumi ya kugombania mradi wa bomba la mafuta ghafi kutoka Uganda kati ya Tanzania na Kenya, wenzetu Kenya walijitahidi kuandika habari zenye kutoa wasifu wa nchi yao ili kuisaidia kupata mradi huo, hivi ndivyo mnavyopaswa kufanya kazi kiuzalendo.”

Aliongeza kuwa leo hii mmeweza kuifahamu TPDC sasa mnapaswa kuwaeleza wananchi miradi inayofanywa na Shirirka hili na manufaa yake katika uchumi wa Taifa, mwende mkatafiti namna mradi wa bomba la mafuta utakavyonufaisha wananchi wanaoishi kando ya njia ya bomba hilo, vilevile namna bomba hilo litakavyosaidia kukuza uchumi wa nchi, hivi ndivyo tunavyoweza kujenga nchi yetu kupitia taaluma ya uandishi wa habari.

Kasesela alisisitiza kuwa ili tujenge Taifa imara ni vyema tuandike habari kwa weledi, uzalendo huku tukiondoa tofauti zetu za kiitikadi ziwe za kikabila, kisiasa au kidini kwa namna hii tutaweza kuandika habari zenye kujenga nchi yetu na si vinginevyo.

Alisisitiza vile vile juu ya utoaji taarifa mapema pale mtu anapoona kuna hujuma au uharibifu wa aina yoyote katika miundombinu hii, akiongea katika warsha hiyo alisema “miundombinu hii ya gesi na mafuta ni mali ya watanzania hivyo kuilinda ni jukumu letu sote kama wazalendo wa nchii hii”.
Akiongea wakati wa ufunguzi wa warsha hiyo, Afisa mahusiano wa Shirika la Maendeleo ya Petroli na gesi Tanzania Maria Mselemu alisema warsha hii inalenga kuendelea kuwajengea uwezo zaidi waandishi wetu wa habari kuweza kuripoti kwa umahiri na ustadi habari za mafuta na gesi.

Mselemu aliwashukuru waandishi wa habari kwa juhudi zao za kuupasha habari umma na kuwaasa kwamba kalamu yao ina nguvu hivyo ni vyema ikaendelea kutumika kujenga uchumi wa Taifa kwa kutoa taarifa sahihi kila wakati.

Katika taarifa yake Faustin Kayombo kutoka mkondo wa juu (TPDC) alisisitiza juu ya matarajio yasiyo halisia yaliyopo miongoni mwa wanajamii na kuwaomba waandishi wa habari kusaidia kuwaeleza wananchi juu ya uhalisia wa sekta.

Kayombo alisema kwamba uwekezaji katika sekta ya mafuta na gesi ni wa gharama kubwa na hata mafaniko kwa maana ya mapato makubwa kwa Serikali huchukua muda mrefu kuonekana.                                                                                                                                                                                                                                                                                                                            
Akitolea mfano mradi mkubwa wa kusindika gesi asilia (Liqufied Natural Gas-LNG), Kayombo alifafanua kwamba itachukua takribani miaka 8 hadi 10 kabla ya mzigo wa kwanza wa LNG kusafirishwa kwenda katika soko la dunia kwa mauzo.
Hata hivyo Kayombo alisisitiza juu ya ushiriki wa wazawa katika sekta hii hususan katika kutoa huduma na kuuza bidhaa.

Naye mwanasheria wa TPDC  Barnabas Mwashambwa alisema sheria mpya ya petroli ya mwaka 2015 inawataka wawekezaji wote kutumia bidhaa zinazozalishwa hapa nchini na kama ikitokea bidhaa hizo hazipo nchini basi kampuni iingie ubia na kampuni ya kizawa ili kuweza kutoa huduma inayohitajika.
Sheria imeeleza kwamba ubia huo lazima umpe mzawa ushiriki usiopunguza asilimia 25%, hii ni fursa kwa wazawa na ni vyema ikachangamkiwa.

Hata hivyo Mwenyekiti wa Waandishi wa Habari mkoa wa Iringa frank leornad ameliomba Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) kutenga muda wa kutosha zaidi katika uelimishaji ili walengwa waweze kuelewa vyema sekta, ombi ambalo liliungwa mkono na Mkuu wa Wilaya.

Katika mafunzo hayo waandishi wa habari walipata fursa ya kujifunza kuhusu maendeleo ya Sekta Ndogo ya Mafuta na Gesi, Matumizi ya Gesi Asilia na Faida Zake, Mradi wa Bomba la Kusafirisha Mafuta Ghafi kutoka Uganda hadi Tanga na Usambazaji wa Gesi Asilia Majumbani, Viwandani na kwenye Vituo vya Kujaza Magari. 
TPDC imeendelea kutoa elimu kwa wadau mbalimbali ikiwa na lengo la kuongeza uelewa zaidi katika sekta hii mpya na changa ya mafuta na gesi hapa nchini.

Saturday, February 18, 2017

HAPPY BIRTHDAY FATHER YOLDA

Huyu ni Padre Wa Shirika la Wa Consolata Ambao wamezindua Jubilei ya miaka 100 tangu Shirika hilo lilipoingia  Tanzania katika Parokia ya Mshindo, Jimbo Katoliki la Iringa. Padri Yolda ndiye mzee kuliko waConsolata wote Tanzania. Padre Jorda, nae ametimiza miaka100 ya kuzaliwa,

Saturday, February 4, 2017

THE COMICS THAT WERE IN STYLE


REMEMBER BARCLAYS BANK IRINGA?

MY NEIGHBOUR GUES WHO?

NOW  when I see him iremember, tikri, iti danti, marbles, migora rugs behind the school, and his pinted shoes

TIMU YA WANAHABARI IRINGA YAPIGWA JEKI NA MBUNGE RITTA KABATI


Mbunge  wa  viti  maalum  mkoa  wa  Iringa Ritta Kabati (CCM) akimkabidhi mwenyekiti wa waandishi wa habari mkoani Iringa moja ya jezi alizotoa kwa waandishi wa habari kwa ajili ya mechi mbalimbali za timu hiyo

 Mbunge  wa  viti  maalum  mkoa  wa  Iringa Ritta Kabati (CCM) ameipiga jeki timu ya wandishi wa habari mkoa wa Iringa kwa kuwapatia   jezi  seti  moja ,mpira na pesa taslim kiasi cha Tsh  50O,000 ili viwasaidie katika malengo yao ya kukipiga ligi daraja la kwanza
.
Na Fredy Mgunda,Iringa

Mbunge  wa  viti  maalum  mkoa  wa  Iringa Ritta Kabati (CCM) ameipiga jeki timu ya wandishi wa habari mkoa wa Iringa kwa kuwapatia   jezi  seti  moja ,mpira na pesa taslim kiasi cha Tsh  50O,000 ili viwasaidie katika malengo yao ya kukipiga ligi daraja la kwanza .

 Akikabidhi  msaada  huo kwa mwenyekiti wa chama cha wandishi wa habari mkoa wa Iringa Frank Leonard juzi    mbunge huyo alisema kuwa  yeye kama mlezi  wa timu hiyo ameamu kujingiza kwa miguu yote kuisaidi timu hiyo ambayo inaonekana kufanya vema kwenye mchezo wa soka mkoani hapo .

Kabati alisema kuwa licha ya kuwa mpira ni ajira pia unamsaidia mtu kuwa na afya njema itakayomsaidia kujiepusha na magonjwa yanayoepukika ikiwemo presha .
“Niwatie moyo hichi mulichokianzisha ni kizuri na timu yenu ina fanya vizuri na juzi tu mumenyakua kombe la Spanest  kwa kuwanyuka kitisi huu ni ushahidi tosha mukiendelea hivi hivi mutakuja kuingia ligi daraja la kwanza na baadaye ligi kuu .

Kabati  aliwataka   wadau  wengine mkoa  Iringa na nje ya  Iringa  kuendelea  kujitolea  kuisaidia   timu   hiyo    ya wanahabari ili iendele kufanya vema ndani na nje ya mkoa wa iringa

Akipokea vifaa hivyo mwenyekiti wa wanahabari mkoa wa Iringa Frank Leonard alimshukuru mbunge huyo kwa vifaa na fedha alizotoa huku akimuahidi mbunge huyo kuwa timu hiyo itakipiga na timu mbalimbali ikiwemo timu ya bunge la jamuhuri wa muungano wa Tanzania

Frank alisema kuwa timu hiyo imekuwa ikifanya vema kutokana na kuwa na wandishi wazuri vijana waliona ari ya kusakata kambumbi hivyo ni vema timu ya bunge kujipanga kisawasa kwani hawata toka salama pindi watakapokipiga nao mjini dodoma

Comments system

Disqus Shortname

Comments System

blogger/disqus/facebook

Disqus Shortname