BINADAMU MZEE KULIKO WOTE AFARIKI DUNIA


Emma Morano
MTU mzee kuliko wote duniani amefariki jana huko Italia, alikuwa na umri wa miaka 117. Emma Morano alizaliwa tarehe 29 Novemba 1899, katika mkoa wa Piedmont, Italia. Alikuwa ndie mtu rasmi wa mwisho ambaye alikuwa amezaliwa katila karne ya 19 ambaye alikuwa hai. Mwenyewe alipokuwa akiulizwa nini kimemfanya aweze kuendelea kuishi mpaka umri mkubwa vile alikuwa akisema siri ni kuwa huwa anakula mayai matatu kila siku, kati ya hayo mawili alikuwa anakula mabichi. Emma alikuwa mtoto wa kwanza kati ya watoto wanane wa baba na mama yake. Emma alikuweko wakati wa vita ya kwanza na ya pili ya dunia.
Daktari wake ambaye amemtibu kwa miaka 27 alisema kuwa mama huyu hakuwa anakula mboga za majani kabisa zaidi alikuwa anakula mayai mawili mabichi asubuhi kisha yai la kukaanga mchana na usiku kipande cha kuku. Kitu kingine ambacho mama huyu alisema kilisaidia kuweza kuishi maisha marefu ni kitendo chake cha kumtimua mumewe aliyekuwa akimnyanyasa, hii ilitokea mwaka 1938, miezi sita baada ya kumzaa mwanae pekee mtoto huyo alifariki basi hapohapo akamfukuza na mumewe ambaye alisema alikuwa hampendi maana mvulana aliyekuwa akimpenda alifariki vitani, na hivyo baada ya hapo hakushughulika kuolewa tena.
Violet Brown wa Jamaica, binadamu mzee kuliko wote aliye hai.
 Kwa kadri ya ya kituo cha Gerontology Research Group (GRG),  mtu mzee kuliko wote duniani kwa sasa ni mama wa Kijamaika  Violet Brown, aliyezaliwa  March 10, 1900.


No comments:

Post Top Ad

Powered by Blogger.