DC KASESELA AWATAKA WANANCHI KUACHANA NA IMANI ZA KISHIRIKINA

 Mkuu wa wilaya ya Iringa Richard Kasesela akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake hii leo

Na Fredy Mgunda,Iringa

Mkuu wa wilaya ya Iringa Richard Kasesela amewataka wananchi wa wilaya ya Iringa kuacha tabia ya kuamini na kujihusisha na maswala ya imani za kishirikina pamoja na kujichukulia hatua mikononi.

Ameyasema hayo baada ya kuwepo kwa taarifa za mtu mmoja mkazi wa kijiji cha Mikong’wi kata ya Kihologota wilaya ya Iringa ameuawa na watu wasiojulikana kwa kukatwa kichwa na kutelekeza kiwiliwili chake.

“Kwanini watu wajichukulie sheria mkononi wakati serikali in jeshi la polisi, mahakama, kuna makanisa na misikiti huku ndio unaweza kutatuliwa shida zako zote.  Na haya mambo ya kishirikina serikali haiamini na nasikitika sana kwa tukio la leo ni baya sana” alisema Kasesela

Kasesela alisema kama wilaya wamepokea taarifa hiyo kwa masikitiko na kuwataka wananchi wote kutojichukulia sheria mikononi kwa kuwa serikali haiamini uchawi na kwamba ameliagiza jeshi la polisi kufanya uchunguzi ili kubaini aliyehusika na tukio hilo.

“Wilaya ya Iringa ilikuwa imetulia sasa yameanza mambo ya kuuwana kwa kweli lazima jeshi la polisi lifanye uchunguzi kwa kina kubaini nini kinachoendelea katika kijiji cha Mikong’wi na lazima tukomeshe na kuwapa elimu wananchi kutojihusisha na maswala ya kishirikina kwa kuwa serikali haiamini sala hilo”alisema Kasesela 

Kasesela ameeleza kuwa tukio hilo limetokea asubuhi ya leo na kumtaja aliyefariki dunia kuwa ni Hasani Nyalusi mkazi wa kijiji cha Mikong’wi tarafa ya Ismani mkoani Iringa.

Aidha Kasesela amewaomba viongozi wa dini mbalimbali kutoa elimu ya Mungu na kukemea maswala ya kishirikina kwa kuwa yanapunguza nguvu kazi za wananchi.


Kwa upande wake, Afisa Mtendaji wa kijiji cha Mikong’wi Majorino Muyinga Anaeleza kuwa mnamo tarehe 06/04/2017 Hassan Nyalusi alikutwa akiwa ameuawa nje ya nyumba yake na mtu au watu wasiofahamika na mwili ukiwa hauna kichwa na uchunguzi wa daktari umefanyika na kukabidhiwa kwa ndugu wa marehehemu kwa taratibu za mazishi, mpaka sasa mtu mmoja, Jackson Nyalusi, anashikiliwa na polisi kuhusishwa na mauaji haya, upelelezi bado unaendelea.
 

No comments:

Post Top Ad

Powered by Blogger.