DKT. JESCA MSAMBATAVANGU ASHIKILIWA NA POLISI


Jesca Msambatavangu
Aliyewahi kuwa Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) mkoa wa Iringa Dkt. Jesca Msambatavangu amekamatwa na polisi kwa tuhuma za kumshambulia mwanamke mmoja na kumpiga ikiwemo kumchoma sindano inayodhaniwa ilikuwa na sumu. Jesca alifukuzwa uanachama wa CCM kutokana kudaiwa kukisaliti chama hicho wakati wa Uchaguzi Mkuu wa 2015. Kamanda wa polisi wa Mkoa wa Iringa Julius Mjengi alithibitisha kuwa jeshi hilo linamshikilia Jesca kutokana na tuhumua za kushirikiana na watu wengine watatu kumvamia mwanamke huyo mkazi wa Kibwabwa nakumpiga sana ikiwemo kumchoma sindano inayodhaniwa ilikuwa ya sumu. Jeshi la polisi linaendelea na msako wa watuhumiwa hao wengine watatu ambao majina yao yamehifadhiwa, ili kufikishwa mahakamani.
No comments:

Post Top Ad

Powered by Blogger.