IFAHAMU IRINGA - 2

Mwaka 1894, Chifu Mkwawa alijenga ngome ya ukuta wenye urefu wa kilomita 8 na kimo cha mita 12, ukuta huu uliojengwa Kalenga ulikuwa ni kwa ajili ya kujitayarisha na vita dhidi ya Wajerumani ambao Mkwawa alijua wangekuja kulipa kisasi baada ya yeye kuwatandika vibaya walipokutana Lugalo. Wahehe wakiwa na silaha hafifu za mikuki na bunduki chache ambazo hawakuwa na uzoefu nazo lakini waliweza kukisambaratisha  kikosi cha jeshi la Wajerumani kilichokuwa na silaha bora zaidi. Hili liliwaudhi sana Wajerumani, kuona Taifa kubwa kama lao kupigwa na kabila moja la Kiafrika. Mwezi Oktoba 1894, Wajerumani wakitokea upande ilipo misheni ya Tosamaganga waliweza kubomoa ngome ya Mkwawa lakini yeye aliweza kutoroka, na kuanzia hapo alianzisha vita ya  guerrilla na kuwasumbua sana Wajerumani kwa miaka mingi, baada ya miaka 9 hatimae waliweza kumzingira lakini aliona bora kujiua kuliko kutekwa na akajipiga risasi. Wajerumani wakakata kichwa chake na kuenda nacho Ujerumani. Fuvu la kichwa hatimae lilirudishwa Uheheni mwaka 1954. Na fuvu hilo lipo katika jumba la maonyesho lililopo Kalenga.
Chief Adam Sapi Mkwawa akipokea fuvu la Chifu Mkwawa

Wahehe wakisherehekea kurudishwa kwa fuvu la Chief Mkwaw 1954

Sherehe za kupokea fuvu la Chief Mkwawa 1954

Sherehe za kupokea fuvu la Chief Mkwawa 1954No comments:

Post Top Ad

Powered by Blogger.