KANISA LINALONYWESHA WAFUASI WAKE BIA LAANZISHWA KONGO


KWA kweli duniani kuna mambo, kumekuweko na makanisa mengi yanaanzishwa kila siku na kila moja viongozi wake wakinadi kuwa wao ndio njia sahihi, kali imeanza huko Kongo, katika jiji la Pointe Noire, kanisa jipya linalojulikana kwa jina la  Louzolo Amour limeanza nalo linahubiri kuwa kunywa bia kunaweza kuondoa mapepo. Kanisa hilo limeanza kupata wafuasi wengi sana. Kanisa hilo lilianzishwa na  Guy Emile Loufoua Cetikouabo, ambaye wanamtangaza  kuwa yeye ndie Mungu na haonekani kwa macho ila anawakilishwa duniani na kiongozi wa sasa  wa kanisa hilo Charles Mikoungui Loundou. Charles huwaambia wafuasi wake kuwa kiongozi wao  Guy Emile Loufoua Cetikouabo alikuwepo, yupo na atakuwepo milele, na kuwa alizaliwa bila kitovu jambo ambalo linaonyesha Umungu wake.

Kanisa hilo linaamini kuwa kunywa bia kwa imani kunaifanya bia iwe “biéramicine”, kitu ambacho kinaweza kuponya maradhi na kuondoa pepo. Ibada za kanisa hili huchukua hata saa 9, watu wakinywa na kusafisha roho zao. 

Mmoja wa waumini, Kondi Jean-Jacqyues alisema,’Nilimleta ndugu yangu hapa alikuwa anaumwa na brother Mikoungui alinipa chupa ya bia, nilipokunywa funda tatu nikapandisha mapepo, baada ya hapo nikajisikia vizuri sana’. 
Kanisa linawafuasi kama 5000 nchini Kongo. Inasemekana umaarufu wake unaongezeka kwa kasi kiasi serikali haina uwezo wa kulizuia. Kwenye miaka ya themanini kanisa lililojiita la Mitume wa Mwisho lilianzishwa Iringa vijijini na kanisa hilo pia lilitumia ulanzi kwa wingi kwa kudai kuwa ni divai. Na pia lilikuwa likiruhusu wakristu wake kuoa zaidi ya mke mmoja. Likaanza kuwa maarufu sana Iringa Vijijini.

No comments:

Post Top Ad

Powered by Blogger.