KIKOSI CHA KUZUIA RUSHWA CHAKAMATA DOLA MILIONI 43 TASLIM KWENYE NYUMBA YA MTU BINAFSIKIKOSI  cha kuzuia rushwa cha huko Nigeria (EFCC), kimegundua zaidi ya dola milioni 43 (kiasi cha Tshs 94,600,000,000/-) kwenye nyumba moja huko Lagos, Nigeria. Kikosi hicho kiligundua fedha hizo baada ya kupigiwa simu na mwananchi mmoja aliye toa taarifa kuwa kuna mwanamke mmoja ambaye kavaa nguo zilizochakaa na chafu lakini alikuwa akionekana anatoa mabegi nje ya nyumba hiyo ambayo iko eneo la watu wenye uwezo. Baada ya kufuatilia, kikosi hicho kilitoa taarifa kuwa pamoja na dola hizo za kimarekani pia kulikutwa fedha za Kinaijeria Naira milioni 23.2 (kisasi cha Tshs 165,000,000/-), Fedha hizo taslim zilikutwa zimepangwa vizuri kwenye makabati ya mbao kwenye chumba cha kulala. Kwa maelezo ya taasisi hiyo fedha hizo zinasadikiwa zilipatikana kutokana na shughuli zisizo za kihalali. Bado hajakamatwa mtu kutokana na fedha hizo. Kwa muda mrefu nchi ya Nigeria imekuwa nchi moja wapo inayohangaika na tatizo la rushwa katika jamii yake. Mafanikio ya kukamata fedha hizi nyingi yametokana na utaratibu mpya uliowekwa na serikali ya Nigeria wa  kumpatia kila anaetoa taarifa za rushwa kati ya asilimia 2.5 hadi 5 ya fedha zinazokamatwa kwenye tukio. Waziri wa Habari wa nchi hiyo alisema kutokana na mpango huo, kufikia mwezi wa pili tayari zaidi ya dola bilioni 180 zilikuwa zimekamatwa. 

WAZO MUAFAKA HATA HAPA KWETU

No comments:

Post Top Ad

Powered by Blogger.