KISIWA CHA ADHABU CHA UGANDA- WASICHANA WALIOPATA MIMBA NJE YA NDOA WALIACHWA HUKO


Kisiwa cha Akampene
“Familia yangu ilipogundua nina mimba, walinichukua kwenye mtumbwi na kunipeleka kisiwa cha  Akampene ( Kisiwa cha adhabu). Kule nikakaa bila kula wala kunywa maji kwa siku nne,” hayo ndio yalikuwa maneno ya Mauda Kyitaragabirwe, ambaye anasema mkasa huu ulimkuta akiwa na umri wa miaka 12 tu.
"Nakumbuka nilikuwa na njaa na nilikuwa nasikia baridi sana, nilikuwa karibu kufa."
Siku ya tano akaja mvuvi mmoja na kusema amekuja kunichukua, nikawa na wasiwasi kuwa nikiingia kwenye mtumbwi wake akifika katikati atanitupa majini. Lakini yeye akasema amekuja kunichukua niende nae kwake, na kuwa ameamua niwe mkewe. Na kuanzia siku hiyo nikawa mkewe. Mume wake huyo amefariki mwaka 2002 na bibi Mauda anasema alikuwa mwanaume mwema na mkarimu sana.
Mauda Kyitaragabirwe anaishi katika kijiji cha Kashungyera nchini Uganda, umbali wa dakika kumi hivi kutoka Kisiwa cha adhabu ambacho ni kisiwa kidogo chenye nyasi na ina unyevunyevu muda wote. Mauda ni bibi Mzee mwenye miaka 106 hivi, yeye anatoka katika kabila la Bakiga ambalo nyakati za ujana wake mwanamke alikuwa anaruhusiwa kupata mimba kama ameolewa tu. Kuozesha binti bikira ilikuwa faida kubwa kwa familia maana mahari ilikuwa juu, ng’ombe wengi walilipwa. Binti kupata mimba nje ya ndoa ilionekana kwanza ni aibu kwa familia na pia ilikuwa inapunguza thamani ya utajiri wa familia. Ili kuondoa aibu familia zilikuwa zikiwatupa binti zao kwenye kisiwa cha adhabu, na kuwaacha wafie huko. Kwa kuwa eneo hili lilikuwa mbali na miji mila hiyo iliendelea muda mrefu mpaka wamisionari walipoingia huko na kuhamasisha iachwe. Kuna sehemu nyingine ya Uganda inayoitwa siku hizi Rukungiri ambapo mabinti waliopata mimba kabla ya kuolewa walikuwa wakiuwawa kwa kusukumwa na kaka zao kwenye miamba mikubwa ya maporomoko ya maji ya Kisiizi, inasemekana mchezo huu ulikuja kuachwa baada ya binti mmoja kumng’ang’ania kaka yake na wote wakaangukia majabali hayo na kufa. Hakuna msichana aliyewahi kusalimika Kisiizi lakini wale walioachwa Kisiwa cha adhabu wengine walinusurika kwani vijana waliowachukua waliweza kuwaoa bila kulipia mahari.
Mauda Kyitaragabirwe akiwa na mjukuu wake
 Kusoma zaidi makala hii ingia HAPA

No comments:

Post Top Ad

Powered by Blogger.