KOMBE LA MSOFU LITASAIDIA KUINUA NA KUIBUA VIPAJI IRINGA VIJIJINI.


 MKOA wa Iringa ni kati ya mikoa iliyobarikiwa hazina kubwa ya vipaji vya michezo mbalimbali lakini vinakosa mwelekeo lakini kupanda kwa timu ya soka ya Lipuli fc ‘Wanapaluhengo’ hadi ligi kuu soka Tanzania bara kumeleta mwamko mkubwa kwa wadau mkoani hapa kuendeleza soka la vijana.

Moja ya wadau waliokitokeza kuanzisha mashindano ya mpira wa miguu ni kampuni ya Jazinga Properties Tanzania Ltd inayomilikiwa na mdau wa soka Jeremia Msofu ambaye kwa sasa ameanzisha mashindano ya kutafuta vipaji vya wachezaji katika wilaya ya Iringa vijijini mkoani Iringa kupitia mashindano ya Msofu Cup.
Mdhamini wa mashindano ya Kombe la Msofu, Jeremia Msofu (kushoto) akikabidhi vifaa vya michezo kwa mmoja ya timu zilizoshiriki mashindano ya Msofu Cup katika Kijiji cha Kiponzelo Kata ya Kiponzelo, Jimbo la Kalenga wilaya Iringa, mkoani Iringa

Mashindano hayo ambayo yamekwisha hivi karibuni kwa timu ya soka ya kijiji cha Itengulinyi kuibuka mabingwa kwa mara ya kwanza ya baada ya kuibwagwa kwa mikwaju ya penati 4 – 3 timu ya soka ya Kijiji cha Kiponzelo katika mchezo wa fainali uliopigwa katika uwanja wa shule ya Sekondari Kiponzelo ulioko katika wilaya ya Iringa.

Katika mashindano hayo mshindi wa kwanza alijipatia shilingi 500,000 mshindi wa pili aliondoka na shilingi 150,000 wakati timu yenye nidhamu ya kijiji cha Usengelindeti walijipatia 50,000. Kipa bora Anuary Japhary aliondoka na shilingi 50,000 na Mfungaji bora alikuwa Adam Kihongosi shilingi 50,000

Mdhamini mkuu wa mashindano hayo kutoka kampuni hiyo ya Jazinga Properties Ltd Jeremia Msofu ambae ni mwananchi wa kijiji cha Kiponzelo kata ya Maboga anasema amelazimika kufanya hivyo kama njia ya kukuza michezo kwa vijana ili kuongeza ajira kwa wale wenye vipaji vya kucheza soka katika wilaya ya Iringa vijijini na kuwapata wachezaji ambao wataweza kuinua soka la mkoa wa Iringa kw ujumla.

Anasema kuwa mashindano hayo yanaendeshwa kwa kushirikiana na chama cha mpira wilayani Iringa na kwa mwaka jana yalianza Desemba 11 na kumalizika Februari 4 mwaka huu. Hivyo kwa mwaka huu yataanza mapema ili kuwezesha wadau mbalimbali kuja kushuhudia vipaji ambavyo vitajitokeza katika mashindao hayo ya kila mwaka.

Jeremia alisema kuwa kupitia mashindano hayo vipaji vingi vitajitokeza na anategemea baada ya mashindano kwa mwaka huu na msimu uliopita itaundwa timu ya Jimbo la Kalenga itakayoweza kucheza kuanzia ligi ya daraja la nne la hadi ligi kuu Tanzania (VPL) kupitia wataalamu watakaochagua wachezaji wenye vipaji kwa kila msimu na kuwekwa katika kambi ya pamoja kuunda timu ya jimbo.

Pia aliahidi kuwa kwa kupitia udhamini wa mashindano hayo, atahakikisha kila timu inapatiwa vifaa vya michezo, kama vile  jezi seti moja na mpira moja kwa kila timu ya vijiji vyote vya kata ya Maboga ambavyo vinashiriki mashindano hayo ya kombe la Msofu.
Mdhamini wa mashindano ya Kombe la Msofu, Jeremia Msofu akizungumza wakati wa msimu wa kwanza wa mashindano ya kombe hilo.
Aidha Msofu alisema kuwa licha ya kudhamini mshindano hayo atahakikisha vijana wote wenye nia ya kupata mafunzo ya urefa watapatiwa udhamini wa masomo endapo wakiwa tayari kwa lengo la kuwazesha kufahamu zaidi sheria za soka pindi wakichezesha mechi mbalimbali zinazojitokeza katika kata ya Kiponzelo na Wasa.

“Wenye nia ya kutaka kuwa marefa wa kimataifa nitahakikisha wanapatiwa mafunzo hivyo wajitokeze na wakiwa tayari basi nitawasaidia kuhusu hili, hii ni moja ya ahadi zangu kwenu vijana lakini siwezi iishia hapa nitaendelea kudhamini mashindano haya kila mwaka kwa lengo lile lile la kukuza vipaji na kuwapata wachezaji watakaoweza kuunda timu ya jimbo’’ Msofu alisema pia, kwa kupitia wadau mbalimbali wa ndani na nje ya nchi atakahakisha mashindano hayo yanakuwa bora kila mwaka na timu mbalimbali za ligi soka Tanzania Bara ziweze kuchukua wachezaji kutoka Iringa hususani wilaya ya Iringa katika tarafa ya Kiponzero


Naye Mratibu wa mashindano hayo, Abuu Changawa ‘Majeki’, ambaye alikuwa Mwenyekiti wa Lipuli FC ya mjini Iringa kabla ya kusimamishwa aliwasisitizia wachezaji wataoshiriki Kombe Msofu mwaka huu kuzingatia nidhamu endapo wana nia ya kufanikiwa katika maisha ya soka.
Majeki anasema kuwa jumla ya vijiji vinane kutoka kata ya Maboga na Wasa vitashiriki mashindano hayo kwa mwaka huu ukiwa ni msimu wa pili na kuvitaja vijiji hivyo kuwa ni Wasa, Usengelindete, Ufyambe na Ikungwe, (kata ya Wasa), Kiponzelo, Makongati, Magunga na Itengulinyi vya kata ya Kiponzelo pia vitashiriki katika kombe hilo.

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Iringa, Richard Kasesela anasema kuwa anatarajia mashindano ya kombe la Msofu yatazalisha vipaji vingi vya wacheza soka kutokana na mwamko ambao umeonekana katika mashindano ya msimu wa kwanza na kumpongeza mdhamini wa mashindano hayo.Kasesela alisema kuwa serikali ya wilaya ya Iringa itahakikihsa inaanzisha mashindano ya mpira wa miguu kwa kila tarafa kwa lengo la kupata wachezaji watakaokuwa wanatumika na vilabu mbalimbali mkoani hapa hasa timu ya Lipuli na kumtaka mdhamini wa mashindano ya kombe la Msofu kuendelea kuunga mkono kuanzisha mashindano mengine ya michezo mbalimbali kwa wilaya hiyo.

Kasesela alisema kuwa imekuwa kasumba kila mdau anayetaka kuanzisha mashindano mbalimbali ya kuibua vipaji vya michezo mbalimbali huwa kunaibuka mambo ya kisiasa na kutoa wito kwa wananchi kuwa waondokane na imani hiyo kwamba kila mtu anayedhamini mashindano mbalimbali basi ana nia ya kutafuta umaarufu hili aje kugombea uongozi wa hapo mbeleni.Kasesela alitoa wito kwa vijana kujikita katika michezo na kuondokana na mchezo wa kubahatisha ambao umeenea kwa kasi kubwa nchini hasa kwa vijana na kuwataka kujishughulisha na michezo mbalimbali ambayo ni ajira tosha kwa sasa duniani.Alimaliza kwa kuvipongeza vyombo vya habari kwa ushirikiano katika kukuza soka la mkoa wa Iringa na kuwa karibu kwa kila jambo linalohitaji kuandikwa kuhusu michezo kwa mkoa wa Iringa na kusema kuwa alikuwa na imani kuwa waandishi wa habari ni watu muhimu sana katika kuwaunganisha wananchi na Serikali hasa katika masuala muhimu yenye maslahi ya nchi kama kuvumbua vipaji vipya.Mdau wa soka kutoka wilaya ya Iringa, Steven George anasema kuwa ifike wakati wazazi na walezi nchini kuwalea watoto wakitambua vipaji walivyo navyo ili viweze kutumika vyema kwa manufaa ya vizazi vya sasa na vijavyo. Steven nae alisema kuwa watu wengi wanawalazimisha watoto wao kusoma mambo ambayo hawana uwezo nao na kuwaacha wakipotea na vipaji ambavyo wanazaliwa navyo na kinachotakiwa ni kuwatambua na kuwaendeleza katika vipaji walivyonavyo ikiwemo soka.

Naye mchezaji bora wa mashindano hayo, Adam Kihongosi alisema kuwa mashindano hayo yanaweza kuwa makubwa endapo wadau mbalimbali watajitokeza kuyadhamini na kutoa pongezi kwa kampuni ya Jazinga kupitia mkurugenzi wake, Jeremia Msofu kuwezesha kufanyika mashindano ya soka katika tarafa ya Kiponzelo.Kihongosi anasema kuwa hii ndio njia bora na sahihi ya kupata wachezaji kwa ajili ya timu zinazoshiriki ligi mbalimbali na kuwataka wadau kujitokeza kusaka vipaji katika maeneo mbalimbali nchini wasibaki tu mijini.

‘’Ninayo furaha ya kuwa mmoja ya washiriki wa mashindano haya ya kila mwaka na nitahakikisha naendeleza kipaji changu cha kufunga, kwani kila nilipokuwa nikicheza mpira wa miguu na nilikuwa na ndoto ya kuwa mchezaji wa timu ya taifa.Kihongosi alisema kuwa kuwepo kwa mashindano ya kombe la Msofu ni njia ya kunifungulia milango ya kutimiza ndoto zangu na kusema kuwa nitaendelea kuongeza bidii pamoja na kuwasikiliza makocha kwa makini nipate mafanikio zaida anasema KihongosiNo comments:

Post Top Ad

Powered by Blogger.