KUINGIA MAREKANI KUNAZIDI KUWA KUGUMU


Nigeria si nchi mojawapo iliyotajwa na Rais Trump kuwa wananchi wake wangenyimwa ruksa ya  kuingia Marekani, lakini raia kadhaa wa nchi hiyo wamejikuta wakinyimwa ruksa ya kuingia nchi hiyo licha ya kuwa na viza halali zilizowafanya waamini kuwa wanaweza kuingia nchini humo. Mfanyabiashara Femi Olaniyi alisafiri mpaka Los Angeles tarehe 21 Februari mwaka huu akiwa na visa inayomruhusu kuingia Marekani kwa miaka miwili. Siku alipofika uwanja wa ndege aliitwa na maafisa  wa uhamiaji na wakamwambia kuwa atatakiwa kuhojiwa ili kuangalia kama amewahi kufanya uhalifu, kwa kuwa hakuwa kufanya uhalifu alikubali. Baada ya mahojiano aliletewa fomu akaambiwa ataie saini, alipoomba muda wa kuisoma kwanza fomu hiyo ikaondolewa. Badala yake akawekwa katika ulinzi wa siku nne, wakati huo simu zake zote zikiwa zimechukuliwa, hatimae viza yake ikafutwa na akarudishwa Nigeria. Na Olinyi si Mnaijeria peke yake aliyerudishwa kwao. Mnaijeria mwingine mkazi wa Lagos,  Francis Adekola ambaye amemaliza masomo yake ya PhD nchini Canada aliposhuka Atlanta akiwa njiani kwenda kwenye harusi ya rafiki yake, anasema aliambiwa asimame pembeni, akapekuliwa na askari aliyekuwa na silaha ambaye alichukua simu yake akasoma meseji zake zote na pia kuangalia picha zote, na akaambiwa na yule askari kuwa ana wasiwasi kuwa akiingia Marekani hatatoka tena hivyo akpandishwa kwenye ndege na kurudishwa Abuja, kilomita 460 kutoka Lagos mji aliokuwa anaishi. Afisa mmoja wa benki Popoola Olayemi anasema alirudishwa na maafisa wa Marekani alipofika Abu Dhabi akiwa na mkewe aliyekuwa mjamzito. Maafisa wa Kimarekani walimkabidhi kwa wafanyakazi wa Etihad wakati huo wamekwisha mnyang’anya passport, na kumrudisha Lagos ambapo ndipo alipogundua kuwa viza yake imefutwa. Waafrika kutoka nchi nyingine pia wanakumbana na kasheshe kama hizo. Mkenya mmoja Ednah Chepkoton alitoa taarifa ya kuzuiwa masaa matatu katika uwanja wa ndege wa  Chicago, O'Hare International Airport na baada ya hapo akarudishwa Kenya. Pia kumekuweko na matatizo ya kunyimwa viza kiasi cha kwamba mkutano mkubwa wa
 African Global Economic and Development Summit umefanyika  Los Angeles mwaka huu bila ya kuwa na washiriki kutoka Afrika kutokana na kunyimwa  viza. Baadhi ya washiriki walionyimwa viza ni kutoka Uganda, Ghana na Nigeria, kwa mujibu wa watayarishaji wa mkutano huo.

No comments:

Post Top Ad

Powered by Blogger.