LIVANGALA AINA NYINGINE YA MUZIKI WA WAHEHE

Ngoma ya Livangala, hutumia njuga (mangala) na ngoma. Njuga huvaliwa miguuni na kwa ustandi huku wachezaji wa kiwa na njuga za milio mbalimbali hucheza na kuleta burudani kubwa kwa mchanganyiko wa muziki wa ngoma (ndusi), njuga na uimbaji. Ngoma hii huchezwa katika sherehe na misiba tofauti inakuwa katika aina ya nyimbo zitakazotumika katika shughuli. Hapa chini ngoma hii ikichezwa kuzunguka kaburi ikiwa ni moja ya mila za Kihehe kumuaga aliyefariki. Wafiwa kuhamasishwa kucheza ngoma ili kukubali yaliyotokea na kuanza kuendelea na maisha.

No comments:

Post Top Ad

Powered by Blogger.