MAANDAMO YA KUMLAZIMISHA RAIS TRUMP KUWEKA HADHARANI HESABU ZAKE ZA KODI-VIDEOKUMEKUWA  na maandamo katika sehemu zaidi ya 150 nchini Marekani, wananchi wa nchi hiyo wanamtaka Rais wao Donald Trump aweke hadharani mahesabu yake ya kodi. Bwana Trump amekuwa Rais wa kwanza kugoma kuweka karatasi zake za kodi hadharani, karatasi ambazo zitaonyesha kama alikuwa mlipa kodi mzuri. Wananchi hao wanataka kujua alifanya biashara na nani, ili kuangalia kama kuna mambo yanaweza kuwa ni kikwazo kwa yeye kuwa Rais asiye na upendeleo wowote. Katika maandamano hayo yaliyotokea
Berkeley, California ngumi ziliumuka kati ya wanaomuunga mkono Trump na wale wanaompinga Trump. Watu zaidi ya 20 walikamatwa na vyombo vya dola. Hakuna sheria inayomlazimisha Trump kuonyesha karatasi zake hizo za kodi lakini utamaduni ulijengwa na marais kabla yake ili kuonyesha walivyo safi mbele ya jamii ya nchi hiyo.No comments:

Post Top Ad

Powered by Blogger.