MASHINDANO YA MAGARI IRINGA KUANZIA TAREHE 22/4/2017



GARI LA AHMED KWENYE MASHINDANO YALIYOPITA

RAMANI YA NJIA ZA MASHINDANO
Rally of Iringa 2017 ndio habari ya mjini Iringa hasa kwa weekend ijayo. Mji huu mkongwe na mzuri  utakuwa na shamrashamra kubwa Iringa kwani kutakuwa na mashindano ya magari maarufu kwa jina la Rally of Iringa 2017, ambayo yatafanyika kuanzia tarehe 22/4/2017. Kwa maaelezo ya watayarishaji, mashindano haya ambayo yatakuwa na route (mizunguko) kadhaa yataanzia katika uwanja maarufu wa Samora Stadium na kuelekea Tumaini University kupitia Kigonzile mpaka Mgongo. Baadaye yataanzia Igingilanyi kuelekea Kiwhele na kutokea Mkwawa University.
Tarehe 23/4/2017 mzunguko utaanza Wenda mpaka Tanangozi, mzunguko mwingine utaanzia Kalenga Darajani na kwenda Ifunda  kupitia Kiponzelo. Kisha Wenda mpaka Ihemi. Baada ya mizunguko ya siku hiyo  magari yatarudi na kufanya service MT Huwel Garage Ipogolo. Mashindano ya mwaka huu yatakuwa na washindani 20 akiwemo mkongwe Gerald Miller wa Arusha, na kutoka Iringa  tutawakilishwa na Hamid Mbatta na Ahmed Huwel. Hiyo ndio Iringa bwana.

No comments:

Post Top Ad

Powered by Blogger.