MBIO ZA MWENGE ZAZINDUA MIRADI YA MAENDELEO KADHAA IRINGAMbio za Mwenge mwaka huu (2017), zimezindua miradi ya maendeleo  kadhaa katika Halmashauri ya Wilaya ya Iringa. Miradi iliyozinduliwa ni;
1.     Kiwanda cha kuongeza thamani ya mazao ya  misitu cha Agora kilichopo katika Kijiji cha Ugwachanya,
2.     Zahanati ya Mangalali iliyojengwa kwa nguvu za wananchi,
3.     Mradi wa maji katika kijiji cha Malinzanga,
4.     Miradi ya kikundi cha vijana cha wajibika katika kijiji cha Malinzanga,
5.     Darasa la Sayansi la kompyuta katika Shule ya Sekondari Idodi,
6.     Klabu ya mapambano dhidi ya rushwa katika shule ya Sekondari Idodi,
7.     Ghala la kuhifadhia mazao katika kijiji cha Tungamalenga,
8.     Kikundi cha vijana cha Mwendokasi kinachojishughulisha na kilimo cha mpunga katika kijiji cha Tungamalenga,
9.     Kikundi cha akina Mama cha Twitange kinachojishughulisha na kilimo cha mpunga katika kijiji cha Tungamalenga,
10.   Ukarabati wa Barabara ya Kalenga-Kiponzelo katika kijiji cha Ibangamoyo
11.   Klabu ya Mapambano dhidi ya dawa za kulevya katika shule ya Sekondari Kalenga.
Kiongozi wa mbio hizo za Mwenge Kitaifa 2017 Amour Hamad amezishauri Halmashauri nchini kutenga maeneo maalumu kwa ajili ya kuanzisha viwanda. Na pia akawashauri wananchi kutumia fursa ya upatikanaji wa umeme katika kuanzisha viwanda vidogo vidogo ili kuwezesha uchumi wa mtu mmoja mmoja na Taifa kwa ujumla.

No comments:

Post Top Ad

Powered by Blogger.