MCHEZAJI WA BORUSSIA DORTMUND AUMIA KATIKA MLIPUKO ULIOTOKEA JIRANI NA BASI LA TIMU HIYO


Marc Bartra mchezaji aliyeumia katika mlipuko huo

Wachezaji wakiwa nje la basi lao baada ya mlipuko

Basi la timu
Mlipuko umetokea karibu kabisa na basi la wachezaji wa timu ya  Borussia Dortmund, huko  Hoechsten  nje kidogo ya jiji la Dortmund, wakati basi hilo likiwapeleka wachezaji wa timu hiyo ya Ujerumani kuwahi mechi yao dhidi ya  AS Monaco katika ligi ya  UEFA Champions League  siku ya Jumanne. Inasemekana kulikuweko na vitu vyenye kulipuka vitatu vilivyowekwa karibu na lilipoegeshwa basi hilo. Marc Bartra, mchezaji kutoka Spain aliumia mikononi kutokana na vioo vilivyorushwa kutokana na mlipuko huo. Basi hilo lilikuwa na watu kati ya 40 na 50 wakiwemo wachezaji, na wasaidizi wengine wa timu. Mlipuko huo ulisababisha kuvunjika kwa vioo katika basi hilo.

No comments:

Post Top Ad

Powered by Blogger.