MJI WA IRINGA WAZIZIMA KWA SHAMRASHAMRA ZA MASHINDANO YA MAGARI

MASHINDANO  ya mbio  za  magari ya Mkwawa Rally of Iringa leo yaliufanya mji wa Iringa uzizime na maduka mengi kufungwa ili kuwapa muda watu kufurika Uwanja wa Samora na wengine kukaa kando ya barabara, ili kuona mashindano hayo. Mashindano yalianzia  kiwanda  cha maji  Mkwawa Pure Drinking Water na kuelekea Uwanja wa Samora ambako watu wengi walikuwa wamekusanyika kuona mashindano hayo. Mashindano hayo yatachukua siku mbili leo tarehe 22 na kesho 23 April 2017. Mashindano yana washiriki 20.


Mkuu wa Wilaya ya Mufindi aliyemuwakilisha Mkuu wa Mkoa alisema mashindano hayo pamoja na kuwa burudani lakini pia ni fursa kwa wakazi wa Iringa kutumia nafasi hiyo kuongeza kipato chao kwa fursa mbalimbali zitakazojitokeza. Mkuu wa Wilaya ya Iringa Richard Kasesela aliwasihi wananchi wa Iringa kuchukua tahadhari wakati wa mashindano haya ya magari ambayo yatakuwa yakikimbia kwa mwendo mkubwa sana.

“Katika barabara zote ambazo magari hayo yatapita, tunaomba watu wasikatize kabla magari hayo hayapita lakini pia tunatoa wito kwa madereva wa bodaboda kutotumia barabara zitakazotumika wakati wa mashindano hayo,” alisema kuu huyo wa wilaya..
Mwenyekiti wa Klabu ya Magari Iringa, Hammid Mbata alisema mashindano hayo yanafanyika kwa mara ya kwanza Iringa katika muda wa miaka 10. Mbata pia alisema mashindano hayo  yameleta  wageni zaidi ya 200 mjini Iringa ni kichocheo cha biashara mbalimbali, na nafasi ya kutangaza utalii na maendeleo ya jumla ya mkoa wa Iringa. Mbata pia alitoa ratiba ya mashindano na kueleza kuwa  siku ya kwanza mashindano hayo yatapita katika vijiji vya Kigonzile, Mgongo, Igingilanyi, Kiwele na kutokea Chuo Kikuu cha Mkwawa huku siku ya pili yatapita vijiji vya Wenda, Kikombwe, Tanangozi, Kalenga, Makongati, Kiponzelo, Ifunda, Mgama na Ihemi. 
Kaimu Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Iringa, Steven Nyandongo alisema katika njia ambazo mashindano hayo yatapita kuna maeneo hatarishi yatakayodhibitiwa kwa usalama.
Picha kwa hisani ya Blog ya Matukio Daima.
Kwa picha zaidi ingia hapa

No comments:

Post Top Ad

Powered by Blogger.