MKUU WA USALAMA WA TAIFA ASIMAMISHWA KAZI NA RAIS WAKE


Mkuu wa Usalama wa Taifa wa Nigeria Ayo Oke amesimamishwa kazi kuruhusu uchunguzi wa mabilioni ya fedha yaliyokamatwa na kitengo cha kuzuia rushwa nchini humo. Siku chache zilizopita  fedha taslimu $43milioni zilikutwa kwenye nyumba moja katika jiji la Lagos. Rais Muhammadu Buhari kamsimamisha kazi mkuu huyo wa usalama ili kupisha uchunguzi kujua alipata fedha nyingi namna hiyo. Baada ya kitengo chake kudai kwamba fedha hizo ni male ya kitengo. Mpaka sasa Oke hajatoa neno lolote, japo afisa mwingine wa kitengo hicho alisema fedha hizo ziliwekwa kwenye nyumba hiyo kwa matumizi mbalimbali ya usalama wa Taifa hilo. Pamoja na sakata  hilo Rais Buhari ambaye aliingia madarakani akiahidi kupambana tatizo la rushwa, amemsimamisha kazi msaidizi wake wa karibu David Babachir Lawal, ili kuchunguza utoaji wa zabuni katika jimbo la Kaskazini Mashariki mwa nchi hiyo, eneo ambalo lina tatizo la  Boko Haram. Kamati ya watu watatu itakayoongozwa na Makamu wa Rais Yemi Osinbajo itachunguza kesi zote mbili. Kamati imepewa siku 14 kumaliza uchunguzi.

No comments:

Post Top Ad

Powered by Blogger.