Mkwawa Rally of Iringa yakamilika Gerald Miller ashinda nafasi ya kwanza

Washindi wa kwanza Gerald Miller na Peter Fox
Babu Gerald Miller na Peter Fox, madreva wazoefu wa mashindano ya magari, wakiwa wanatumia gari aina ya Mitsubishi Evo IX, wameshinda mashindano ya Mkwawa Rally Of Iringa 2017 kwa kuwa wa kwanza katika mashindano haya. Washindi wa pili walikuwa Randeep Singh na Zubayr Piredina katika gari aina ya Mitsubishi Evo IX, washindi wa tatu Dharam Pandya na Awadh Bafadhi nao wakitumia gari ya aina hiyohiyo. Madreva wa Iringa wameshindwa kutamba hakuna hata aliyekuwa katika tano bora. Mkongwe Ahmad Huwel akiwa na Maisam Fazal wamekuwa wa saba, wakati Hamid Mbata na Sultan Chana wakiwa wa tisa. Mkongwe mwingine wa mashindano haya Frank Taylor akiwa na George Manyai wamekuwa wa kumi.


Washindi wa Pili

Washindi wa tatu

Matokeo

No comments:

Post Top Ad

Powered by Blogger.