MKWAFI MNYAKIDADA

Friday, April 21, 2017

POLISI AUAWA KWA RISASI KATIKATI YA JIJI LA PARIS


Polisi wakiwa lindoni mda mfupi baada ya tukio
Polisi mmoja ameuwawa na wengine wawili wamejeruhiwa katikati ya jiji la Paris Ufaransa na mtuhumiwa wa mauaji hayo aliuwawa muda si mrefu baada ya hapo. Mtuhumiwa huyo aliyekuwa peke yake inasemekana alishuka kwenye gari alilokuja nalo na kuanza kulifwatulia risasi basi lilikuwa na  polisi na kisha kuanza kukimbia huku akipiga risasi ambapo aliwajeruhi askari wawili,  lakini alitwangwa risasi na kufa hapohapo. Rais wa Ufaransa Francois Hollande alisema ana uhakika tukio hilo ni la kigaidi. Muda mfupi baadae kundi la IS kupitia shirika lake la utangazaji Amaq News lilimtaja mtuhumiwa kuwa ni Abu-Yusuf al-Baljiki, na kuwa alikuwa mmoja wa wapiganaji wake. Serikali ya Ufaransa ilisema inamtambua mtuhumiwa lakini haikutaja jina lake kwa kuwa uchunguzi ulikuwa unaendelea

No comments:

Post a Comment

Comments system

Disqus Shortname

Comments System

blogger/disqus/facebook

Disqus Shortname