WANGONI WATANI WA JADI WA WAHEHE

WANGONI ndio kabila ambalo ni watani wa jadi wa Wahehe, moja ya sababu ambazo hutajwa kuwa sababu ya utani huu ni kuwa katika vita za kikabila zilizokuwa zikiendelea kabla ya ujio wa wakoloni, Wahehe na Wangoni waliwahi kupigana na hakukupatikana mshindi, na kuanzia hapo walianza utani kila moja akitamba kuwa bora kuliko mwenzie. Utani wa makabila haya mawili ni utani wenye heshima watu wa rika moja ndio ambao hutaniana, hauhusishi matusi kama ulivyo utani wa baadhi ya makabila. Na utani huu hugeuka nyenzo muhimu ya kusaidiana wakati wa misiba ambapo watani husaidia kukusanya michango na kufanya kazi ambazo zinawapunguzia mzigo wafiwa.

No comments:

Post Top Ad

Powered by Blogger.