WATURUKI WAPIGA KURA ZA MAONI KUAMUA RAIS APEWE MADARAKA ZAIDI


Istanbul, Turkey –  Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan amefurahia matokeo ya kura za maoni ambapo watu wa Uturuki wameamua kumuongezea Rais wa nchi yao madaraka makubwa katika utendaji wake. Mabadiliko hayo ambayo yanaungwa mkono na  Erdogan, na chama cha Justice and Development Party (AK Party), chama ambacho alikianzisha, pia yanaungwa mkono na uongozi wa  Nationalist Action Party (MHP), chama ambacho kilimuunga mkono Bungeni kuwezesha kufanyika kwa kura hizo za maoni.
Waziri Mkuu wa nchi hiyo Binali Yildirim nae aliwashukuru sana wananchi wa Uturuki kwa uamuzi wao huo. Kufikia saa sita mchana jana Jumapili, waliopiga kura za ndio kumpa madaraka zaidi Rais walikuwa asilimia 51.3. Asilimia 99 ya kura zilikuwa zimesha hesabiwa. Kutokana na matokeo ya kura hizo Katiba ya Uturuki itabadilisha uongozi sasa na maamuzi yataondolewa kwenye Bunge na kupewa Rais. Hivyo kumpa uwezo mkubwa sana Rais wa nchi hiyo. Matokeo haya yataanza kutumika mwaka 2019  baada ya uchaguzi mkuu wa nchi hiyo.
Wanachama wa chama tawala walikuwa wanasifia uamuzi huo ambao wanaamini utamuwezesha Rais wao afanye makubwa zaidi kwa nchi yao. Wakati huohuo chama kikuu cha upinzani cha nchi hiyo The Republican People's Party (CHP) kimeyakataa matokeo hayo na kudai lazima kura zihesabiwe upya kwenye asilimia 60 ya maeneo. Chama hicho kimelaumu utaratibu uliokubaliwa dakika za mwisho wa kuruhusu karatasi zilizokosa muhuri halali kuruhusiwa kutumika kwenye upigaji kura. Wapinzani walianza kupita mitaani wakipiga masufuria na sahani, njia ambayo hutumika nchini humo kuonyesha kupinga kitu
Nchi nyingine za magharibi zinasema kura hiyo ni wananchi kupiga kura kuchagua udikteta

No comments:

Post Top Ad

Powered by Blogger.