ZIMBABWE YASHEREHEKEA MAKA 37 YA UHURU


RAIS  Robert Mugabe wa Zimbabwe amewaambia wananchi wake kuwa miaka 37 baada ya kupata uhuru wananchi wa nchi hiyo wana maamuzi kamili kuhusu nchi yao. Rais huyu mwenye umri wa miaka  93 aliongea haya wakati wa sherehe za miaka 37 ya uhuru wa Zimbabwe. Pamoja na sherehe na shamra shamra kiongozi wa chama cha upinzani cha Movement for Democratic Change (MDC-T) Morgan Tsvangirai alisema, “Siku hiyo ni kumbukumbu tu ya siku ya kupata uhuru lakini siyo siku ya kusherehekea uhuru” Aligusia umaskini uliokithiri, na kusema hali waliyonayo sasa si ile waliyoitegemea wakati wa kupigania uhuru wa nchi hiyo.
Msemaji wa chama cha People’s Democratic Party (PDP), Jacob Mafume, alisema Wazimbabwe hawana kitu cha kuonyesha kwa uhuru unaosherehekewa. Alisema, uhuru wa kisiasa haupo, kuna sheria nyingi zinazoweza kukupeleka mahakamani kutokana na imani yako tu, tena akasema wale wanaopelekwa mahakamani ndio wenye bahati maana wengine wanapigwa na kusulubiwa au kunyimwa chakula bila kufikishwa hata mahakamani. Uchaguzi mkuu ujao Zimbabwe utakuwa  July 2018.

No comments:

Post Top Ad

Powered by Blogger.