AIR ZIMBABWE YAPIGWA MARUFUKU ANGA ZA UMOJA WA ULAYA(EU)


Air Zimbabwe imepigwa marufuku kuruka katika anga za nchi za umoja wa Ulaya (EU). Uongozi wa kampuni hiyo aliiambia BBC kuwa unafanya kila jitihada amri hiyo ifutwe mapema  iwezekanavyo, lakini waziri wa usafiri wa Zimbabwe alikuwa na hadithi tofauti aliyoitoa kwa gazeti la serikali la nchi hiyo The Herald. 
Uongozi wa Air Zimbabwe ulisema unafanya mabadiliko ya kuifanya kampuni hiyo iwe ya kisasa zaidi, kulingana na taratibu za siku hizi za uendesha wa kampuni za ndege, lakini Waziri wa Usafirishaji na Miundombinu Dr. Joram Gumbo, amesema ni ndege mbili tu ambazo zimezuiliwa kwa muda kufanya shughuli katika nchi za Ulaya. Waziri huyo alisema shirika linaloshughulika na usalama wa ndege, European Aviation Safety Agency (EASA), liliona mapungufu mawili tu katika vifungu 12 vya vigezo vilivyoangaliwa. Shirika limepewa muda mpaka mwezi wa 11 liwe limerekibisha mapungufu yake. Air Zimbabwe ambayo ni mali ya serikali inadaiwa kiasi cha  $milioni 300, hivyo kuwa katika hali mbaya.
 Kati ya mashirika ya ndege ambayo yamekumbwa katika panga la kuziwa kuruka katika anga za nchi Umoja wa nchi za  Ulaya (EU) ni Air Zimbabwe,  Aseman Airlines (Iran), Iraqi Airways (Iraq), Blue Wing Airlines (Suriname), Med-View Airlines (Nigeria), Mustique Airways (St Vincent and the Grenadines), Aviation Company Urga (Ukraine). Mpaka tarehe 16 May 2017, mashirika 181 ya ndege yamezuiwa kuruka Ulaya. Ndege za Benin na Mozambique zimeweza kufanya marekibisho na kuruhusiwa kuanza kuruka tena Ulaya. Mwezi Oktoba mwaka jana, Wazimbabwe walitumia mitandao ya jamii kulaani kitendo cha Air Zimbabwe kumchagua mkwe wa Rais Mugabe, Simba Chikore, kuwa Chief Operating Officer (COO) wa shirika hilo. Simba ni mume wa Bona, binti pekee wa Rais Mugabe.

No comments:

Post Top Ad

Powered by Blogger.