BINTI ALIYETUMWA NA BOKO HARAM KUJILIPUA AOKOLEWA NA KUELEZA MKASA WAKE SOMA HAPA


BINTI  wa miaka 14 aliyekamatwa karibu na kituo cha jeshi la Nigeria la Maiduguri, akihisiwa kuwa ametoka kwenye kundi la Boko Haram, kwa nia ya kujilipua ili kulipua kituo hicho, amelieleza shirika la habari la NAN- News Agency of Nigeria (NAN) – kuwa alitumwa kujilipua akiwa kavishwa vitu vya mlipuko baada ya kukataa kuolewa na wanaume watatu kutoka kundi hilo la Boko Haram. Msichana huyo alisema aliishi kwenye kundi hilo kwa miaka mitatu baada ya kutekwa yeye na baba yake huko Borno mwaka 2013, wakati wakiwa mbioni kuokoa maisha yao.
 Yafuatayo ni maelezo ya binti huyo, ambaye jina lake halijatajwa, aliyoyatoa kwa waandishi wa NAN.

 Nimekwisha ishi miaka mitatu mikononi mwa Boko Haram. Wanaume watatu wa Boko Haram walitaka kunioa nikawakataa, wawili kati hao walikuwa viongozi(amir). Nilipokataa kwa mara ya tatu kiongozi moja alikasirika sana na kusema ataniua mimi na baba yangu, mimi nikasema heri kufa kuliko kuolewa na Boko Haram. Baada ya hapo wakasema kwa vile sitaki kuolewa basi watanipeleka Maiduguri kwa ajili ya kujitoa mhanga. Nilikamatwa na na wanaume watatu, wakanipiga sindano na baada ya hapo sikuelewa tena nini kinaendelea. Niliamka nikiwa kwa mganga wa kienyeji ambaye alinambia kuwa nilikuwa kwake kwa siku 30 na ananitayarisha kwa ajili ya kazi maalumu. Baada ya hapo nikaja kuchukuliwa na Boko Haram watatu ambao walikuja na na mvulana na msichan ambaye nao walipitia nilichopitia. Tukashinda siku nzima barabarani tukielekea Maiduguri, tulipofika ndio tukavalishwa mabomu nikajua kuwa saa ya kufa imefika nikaanza kulia. Nikamuona yule msichana mwenzangu akikaribia kituo cha polisi na kujilipua, akafa peke yake, yule mvulana aliuwawa na askari kabla hajajilipua. Kitu kinanambia nivue ile milipuko nikavua na mara moja askari wakanizunguka nikazimia. Nilipoamka nikagundua kuwa mmoja wa wle polisi walionikamata alikuwa mjomba wangu labda ndio maana niko hai.

No comments:

Post Top Ad

Powered by Blogger.