BOMU LA MKONO LAUWA WATATU BURUNDI


Mtu asiyejulikana alitupa bomu la mkono kwenye nyumba moja mjini Bujumbura, na watu watatu ambao inadaiwa ni wanachama wa Umoja wa Vijana wa chama tawala CNDD FDD, wameuwawa. Mpaka sasa watu 700 wameuwawa nchini Burundi, katika vurugu zinazohusisha wanaompinga rais na wanaomuunga mkono,hii ni kuanzia  April 2015 wakati President Pierre Nkurunziza  alipotangaza nia ya kugombea tena Urais. 
Katika tukio la kurusha bomu, watu wengine watatu wamejeruhiwa akiwemo mwanamke mmoja na mwanae, na mwanaume mmoja ambao walikimbizwa hospitali. Msemaji wa polisi Pierre Nkurikiye, alisema kuwa wote waliofariki walikuwa wanachama wa umoja wa vijana wa  CNDD FDD, akiwemo kiongozi wa kitongoji hicho. Watu watano wamekwisha kamatwa akiwemo mmoja ambae ni raia wa Rwanda. Umoja wa Mataifa ulitoa tamko mwezi uliopita ukionyesha wasiwasi wao kuhusu mambo yanayofanywa na vijana wa  CNDD-FDD wanaojulikana kama Imbonerakure, ambao huingia kwenye nyumba za wapinzani usiku na kufanya fujo. UN ilitaka vyombo husika kuzuia taratibu hizo.

No comments:

Post Top Ad

Powered by Blogger.