EBOLA YATINGA TENA KASKAZINI MASHARIKI MWA JAMHURI YA DEMOKRASI YA KONGO


Shirika la Afya Duniani (WHO), limetangaza kuwa Ebola imeingia Kaskazini Mashariki mwa Jamhuri ya Demokrasia ya Kongo. Tangazo hili limekuja baada ya watu 9 kuugua homa yenye kila dalili za Ebola, watatu wamekwisha fariki na mmoja amepimwa na kuhakikiwa kuwa anaugua Ebola. Ugonjwa huu umezuka katika jimbo la Bas-Uele, kaskazini mwa nchi hiyo. Uhakika wa vipimo hivyo ulifanywa katika maabala ya hospitali ya rufaa ya Taifa jijini Kinshasa. Kuanzia sasa WHO  imesema itasaidiana na Wizara ya Afya ya DRC kuhakikisha kuzuia kusambaa kwa ugonjwa huu. Mara ya mwisho Ebola iliingia Kongo mwaka 2014 na watu 50 walikufa kwa maradhi hayo. Ufanisi wa WHO katika kufuatilia ugonjwa huu safari hii, kunachukuliwa kuwa ni marekebisho baada ya kupata ripoti mbaya mwaka 2015, kuhusu utendaji wa shirika hilo katika kukabiliana na ugonjwa huo mwaka 2014 uliposababisha vifo vya watu 11,000 huko Afrika ya Magharibi.           

No comments:

Post Top Ad

Powered by Blogger.