HATIMAE IVAN SSEMWANGA AZIKWA


NOTI ZIKIWA ZIMETUPWA NDANI YA KABURI LA SSEMWANGA KABLA MWILI WAKE HAUJASHUSHWA HUMO
 Ivan Ssemwanga aliyezaliwa Desemba 12, 1977 , amezikwa leo kwenye eneo la  makaburi ambako pia walizikwa mababu zake  huko wilaya ya Kayunga. Ssemwanga aliondoka Uganda mwaka 2002 kuelekea Afrika ya Kusini kutafuta maisha, na huko kwa msaada wa binamu yake aliweza kuanza maisha mapya. Hakuna anaejua hasa Ivan alipataje utajiri, lakini kuna fununu nyingi ikiwemo kuwa alikuwa mganga wa kienyeji ambaye alikuwa akiwahudumia watu matajiri. Kuna wanaosema Ivan na kundi lake waliokuwa wakiijita ‘The Rich Gang' walikuwa ni makawala wa viongozi mafisadi, na hivyo kupata mgao kutokana na mapato hayo. Lililowazi ni kuwa Ivan alikuwa na pesa wakati wowote, na hakuona shida kuzionyesha. Pia alikuwa mtu mwenye kugawa fedha bila hiyana. Mwaka 2010, alilipa mahari ya roli zima la ng’ombe wakati wa kumuoa Zari. Wakiwa na Zari walikuwa na biashara Uganda na Afrika ya Kusini ambako alikuwa na majumba kadhaa ya kifahari Pretoria na Sandton. Pia aliwahi kutoa msaada mkubwa wa kifedha kwenye kituo cha  kulea watoto cha  Nsambya, aliwahi pia kugawa fedha kwa timu ya soka ya Taifa ya Uganda, Uganda Cranes.
Vijana wenye pesa Uganda walifanya shughuli ya mazishi ya Ivan kuwa sehemu ya mashindano ya kuonyeshana utajiri. Siku moja kabla ya mazishi ilionekana kama kila mmoja alikuja na gari lenye jina lake badala ya namba za gari, na magari hayo yakiwa yale yenye bei mbaya.  Kabla mwili wa Ivan haujawekwa kaburi waombolezaji walimwaga fedha za Uganda na Dola za Kimarekani ndani ya kaburi la kijana huyu tajiri. 
Ujumbe ulioandikwa na watoto wa Ivan hakika uliwatoa machozi wengi waliokuwa wakimfahamu kijana huyu. Watoto hao waliandika maneno yafuatayo;
ZARI na wanae watatu aliozaa na marehemu Ivan Ssemwanga
 
 “Dad, so many thoughts come to our mind whenever we speak of your name; it seems without you in our lives things will never be the same. We think of the good old days when we were still so little; consumed in your love, and in your smile.”
“Those days are gone and no matter what we do, life will never be the same! Oh Dad, if only we could turn back the hands of time and hear your voice once more, but God called you to a better place, so peaceful and free of pain. And when we see you sleeping, we can only wish the best for you.”
    REST IN PEACE IVAN SSEMWANGA

No comments:

Post Top Ad

Powered by Blogger.