JACK PEMBA MBARONI UGANDA


Jack Pemba akiwa na Kofi Olomide
YULE mfanyabiashara ambaye biashara yake haijulikani lakini alikuwa na fedha za kufuru  Jack Pemba, ametiwa mbaroni na polisi wa Uganda katika uwanja wa ndege wa Entebe katika jaribio la kuondoka nchini humo, ambamo mmekuwa makao yake kwa siku za karibuni. Jack Pemba anadaiwa kukamatwa kutokana na amri ya mahakama japo polisi hawakuwa wawazi kuhusu kosa halisi lililofanya itolewe amri hiyo. Msemaji mmoja wa polisi AIGP Asan Kasingye aliwaambia waandishi kuwa Jack Pemba amekamatwa kutokana na upelelezi kuhusu tuhuma za utakatishaji wa fedha. Jack Pemba amekuwa na tabia ya kumwaga fedha hovyo japo hakuna aliyekuwa akijua anazipataje. Angalia video ya Jack akizindua gari lake jipya kwa champagne. Alikuwa mfadhili mzuri wa michezo na wasanii. Kati ya wasanii walioja fedha za jamaa huyu ni  Kofi Olomide na Jose Chameleon, pia aliwahi kufadhili mipira kwa Shirikisho la vyama vya mpira la Uganda (FUFA). Inadaiwa kuna upelelezi wa utapeli wa zaidi ya dola 700,000 (kama TSHS 1,540,000,000) ambazo inadaiwa alimtapeli mfanya biashara kutoka Ulaya anaeitwa Steve Stavropolise, kwa kuahidi kuwa angempelekea dhahabu na shaba za thamani hiyo lakini akachikichia na fedha hizo, jitihada zote alozofanya mzungu huyo za kumshawishi aidha arudishe fedha au apeleke mzigo zilishindikana na hivyo kumfanya Steve kuamua kutumia vyombo vya dola ikiwemo Interpol.

No comments:

Post Top Ad

Powered by Blogger.