JE, RAIS TRUMP ALISHAWISHI UPELELEZI DHIDI YA MSHAURI WAKE MKUU UACHWE?


RAIS TRUMP AKIWA NA FLYNN
Ile tamthilia tamu ya Rais Donald Trump leo imeingia katika awamu nyingine baada ya taarifa mpya kuanza kusambaa kuwa Rais aliwahi kumwambia Mkurugenzi Wa FBI James Comey aache kupepeleza mahusiano kati ya Urusi na  aliyekuwa mashauri mkuu wa Rais Michael Flynn.  Kwa maelezo yaliyopo Rais alimtumia ki memo Mkurugenzi wa FBI kilichosema "I hope you can let this go," kimemo hiki kilikuja siku moja baada ya mkutano kati ya Rais na Mkurugenzi huyo February mwaka huu. Ikulu ya Marekani imekataa katakata kuhusu tukio hilo na kuongeza kuwa Rais hajawahi kumomba Comey wala mtu yoyote kuacha kufanya upelelezi kuhusu General Flynn. Mbunge mmoja wa chama cha Republican Jason Chaffetz, ambaye ni mwenyekiti wa House Oversight Committee, ameitaka FBI kukabidhi nyaraka zote zenye mawasiliano kati ya Rais na Comey kufikia tarehe 24 mwezi huu. Soma hapa    Itakumbukwa kuwa Flynn alitimuliwa kazi kutokana na kosa la kumdanganya makamu wa Rais kuhusu mazungumzo yake na Balozi wa Urusi.
Wakati huu umeanza kuwa mgumu kwa Wabunge wa Republican, kwani wanaona Rais wao kila siku ana zigo jipya…………..  Tamthilia inaendelea

No comments:

Post Top Ad

Powered by Blogger.