JOHN KITIME NA ANAIA NGOLIGA JUKWAANI IRINGA NA DAR ES SALAAM

JUMAPILI- 21  May 2017, John Kitime atakuwa jukwaani na gitaa lake, akiburudisha kwenye tamasha la Isimila Music Festival, litakalofanyika weekend hii Iringa. Atakuwa jukwaani kuanzia saa 8:45 mchana. Tamasha hili linafanyika eneo ambalo waliwahi kukaa watu wa kale "Enzi ya Mawe". Wahenga watapata burudani.
JUMANNE- 23 May 2017, Anania Ngoliga na John Kitime, kwa pamoja watakuwa jukwaani kutoa burudani yao ya muziki wa kalimba na gitaa. Shughuli itafanyika Nafasi Art Space, Mikocheni Dar es salaam mtaa wa Eyasi, kuanzia saa 9 mchana. Burudani hii itakuwa na vikundi vingine kadhaa usikose burudani hii.

No comments:

Post Top Ad

Powered by Blogger.