JOSEPH KABILA ATANGAZA BARAZA JIPYA LA MAWAZIRI


Rais Joseph Kabila
Rais Joseph Kabila wa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo, jana Jumanne alitangaza serikali mpya ya mpito kuelekea uchaguzi mkuu. Kabila ambaye yuko madarakani kuanzia mwaka 2001, mwezi Desemba mwaka jana aliweza kuingia katika makubaliano ya vyama vikuu vya upinzani kuendelea kuwa madarakani mpaka mwisho wa kipindi chake mwishoni mwa 2017. Katika taarifa iliyosomwa kwenye televisheni ya taifa majina 60 ya mawaziri na manaibu waziri yalitangazwa na mengi ni majina ya majina hayo ni yale yaliyokuweko katika serikali iliyopita. Wizara nyeti kama Wizara Mambo ya Nje, Wizara ya Mambo ya Ndani, Sheria na Migodi ziliendelea kushikiliwa na wanaomuunga mkono Kabila.
Nchi hiyo imo katika matatizo ya kiuchumi kwani fedha ya huko imepungua zaidi ya nusu ya thamani yake katika  miezi michache iliyopita, na serikali ina mtihani wa kukusanya fedha za kuwezesha nchi hiyo kufanya uchaguzi wake mkuu mwisho wa mwaka.

No comments:

Post Top Ad

Powered by Blogger.