KAMA ULIKUWA UNAONA MICHAEL JACKSON ALIKUWA 'CHIZI' BASI BINTI YAKE NDIO ZAIDI


PARIS JACKSON
KAMA  ulikuwa unadhani Michael Jackson alikuwa wa ajabu ajabu basi ni wazi binti yake amerithi hali hiyo. Paris Jackson mwenye umri wa miaka 19, binti pekee wa marehemu Michael Jackson ambaye kwa sasa anafanya shughuli za ‘umodo’, hivi karibuni kwa kupitia ukurasa wake wa instagram aliweka picha yake inayomuonyesha alipigwa picha hiyo bila nguo pembeni yake kukiwa na mbwa wake lakini akaweka vi emoji vya kuhifadhi chuchu zake, akaandika katika ujumbe huo kwa followers wake milioni 1.4 maneno yafuatayo "nudity is natural and part of what makes us human". Watu wengi hawakufurahishwa na picha hiyo na kumpa vipande vyake mpaka akaondoa picha hiyo lakini akaweka picha yake nyingine akiwa hajavaa kitu kuanzia tumboni huku akivuta sigara, na akaandika, "kukaa utupu hadharani kunasaidia mtu kujiunga na ulimwengu na vitu vyake vilivyo vizuri", mwisho akamaliza  "If this makes some of you upset i completely understand and i encourage you to maybe no longer follow me, but i cannot apologize for this in any way. it is who i am and i refuse to shy away and keep my beliefs a secret."
Paris alikuwa na umri wa miaka 11 tu baba yake alipofariki tarehe 25 June mwaka 2009. Binti huyu wa superstar  aliwahi kusema kuna wakati mwaka 2003 aliwahi kujaribu kujiua. Ni wazi huyu ‘chizi’ zaidi ya babake

No comments:

Post Top Ad

Powered by Blogger.