KIJANA WA MIAKA 22 AJILIPUA NJE YA UKUMBI WA MUZIKI NA KUUWA WATU 22


WATU 22 wameuwawa na 59 wamejeruhiwa wengine wakiwa wamejeruhiwa vibaya sana. Mkasa huu umetokea baada ya kijana wa miaka 22, Salman Abedi alipojilipua mwishoni mwa onyesho la muziki uliokuwa unaporomoshwa na muimbaji wa Kimarekani Ariana Grande onyesho lililofanyika  Manchester Arena, katika jiji la Manchester kule Uingereza. Polisi wa huko walisema, Salman alijilipua kwa bomu lililotengenzwa nyumbani, alipojitegesha kwenye kibaraza cha ukumbi huo na kujilipua wakati vijana wengi wakiwa wanatoka kwenye onyesho hilo. Bomu hilo ambalo linaonekana lilitengenezwa kwa kujazwa misumari na vyuma vyuma ambavyo vilisambaa eneo la tukio, limeuwa hata watoto wadogo wa chini ya miaka 16 ambao walikuwa wamesindikizwa na wazazi wao kwenye onyesho hilo. Muuaji alikufa palepale. Salman alizaliwa Manchester siku ya mwaka mpya 1994, inasemekana ana kaka yake mkubwa aliyezaliwa London na ndugu zake wadogo msichana na mvulana waliozaliwa Manchester. Familia hiyo yenye asili ya Libya, imeishi Uingereza kwa miaka mingi sana.
Watu wa madhehebu mbalimbali wakionyesha uchungu wao, kwa waliofariki Manchesters
Kundi la ISIS limeshadai kuwa limehusika katika janga hilo. Waziri Mkuu wa Uingereza Thereza May, ametangaza kuiweka nchi yake katika hali ya hatari, hii inatokana na kuwa bado haijajulikana kama Salman alikuwa peke yake au alikuwa na watu wengine ambao bado hawajakamatwa. Tayari kijana mwingine wa miaka 23 amekamatwa kwa kushukiwa na kuhusika na tukio hilo.
Serikali hiyo imetangaza kuwa kuanzia sasa wanajeshi wataanza kuonekana kwenye maonyesho ya muziki. Serikali imeweka simu namba 0800 789321 kwa yoyote mwenye taarifa kuhusu ugaidi wowote.

No comments:

Post Top Ad

Powered by Blogger.