MARAIS WAWILI WA AFRIKA WAELEKEA NCHI ZA NJE KWA MATIBABU WIKI HII


Rais Robert Mugabe wa Zimbabwe, ambaye sasa ameshatimiza miaka 93, jana Jumatatu amekwenda Singapore kupima afya yake. Mara ya mwisho alienda huko ilikuwa mwezi March mwaka huu. Afya ya Mzee Mugabe imekuwa ni gumzo huko Zimbabwe, vyama vya upinzani vikidai afya ya mzee huyu ni mbaya na ana matatizo ya kansa, wakati wasaidizi wa Rais wakikataa tuhuma hizo na kusema kuwa ameenda kutibiwa tatizo la macho. Mwaka 2018 kuna uchaguzi mkuu nchini Zimbabwe na Mzee Mugabe ndie chaguo la chama chake kugombea kwa mara nyingine wadhifa huo, ambao kaushikilia toka mwaka 1980, akiwa Waziri Mkuu.

Nae Rais wa Nigerian  Muhammadu Buhari, ameondoka nchini mwake Jumapili kuelekea Uingereza kwa ajili ya kupima afya yake, kwa maelezo ya msemaje wake, Femi Adesina,   Rais Buhari atakaa Uingereza kadri ya maelekezo ya daktari wake, na kuwa serikali itaendeshwa na makamu wa Rais. Hii ni mata ya pili kwa Buhari mwenye miaka 74 kurudi Uingereza kwa matibabu mwaka huu, nae afya yake imekuwa gumzo nchini mwake.

No comments:

Post Top Ad

Powered by Blogger.