MATATIZO YA KIRUSI WANNACRY KUONGEZEKA JUMATATU-DUNIA HAIJAPATA JIBU


Nchi zilizokumbwa na kadhia ya kirusi cha WannaCry
MATATIZO yaliyoikumba mitandao ya kompyuta zaidi ya 125,000 hadi kufikia Ijumaa, yatawezekana kuongezeka na kuwa mabaya zaidi kuanzia Jumatatu, wataalamu wa usalama wa mambo ya mitandao wametangaza. Kijana mtaalamu ambaye ameweza kufanikiwa kupunguza kuendelea kusambaa kwa kirusi kilichoingilia maelfu ya kompyuta dunia nzima  amesema kirusi kingine chenye nguvu zaidi kitaweza kusambazwa Jumatatu.
Wachunguzi wanahangaika kuwatafuta wahalifu walioweza kuingiza kirusi hiki ambao kwa sasa wanadai malipo ya kati ya dola 300-600 ili kuondoa kirusi hicho kwenye kompyuta. Mitandao iliyokuwa ikitumia mfumo wa Microsoft Windows ndio hasa iliyopigwa na kirusi hiki kilichoitwa WannaCry au Wann Decryptor

No comments:

Post Top Ad

Powered by Blogger.