MAZISHI YA IVAN SSEMWANGA YAMEPANGWA KUFANYIKA JUMANNE


Ndugu wa marehemu Ivan Ssemwanga wanasemeka watachinja ng’ombe watano na wametenga milioni 150 za Uganda kwa ajili ya kununua pombe  wakati wa msiba na mazishi ya ndugu yao huyo. Wasanii maarufu wanaowika siku hizi pia wataalikwa kutumbuiza wakati wa msiba nyumbani kwa marehemu Muyenga na pia kutumbuiza makaburini wakati wa mazishi, kikijiji kwao Nakaliro, wilaya ya Kayunga. 
Mwenyekiti wa kamati ya mazishi Joseph Lutalo Bbosa amesema shughuli nzima itakuwa si msiba, lakini sherehe ya kufurahia maisha ya shujaa aliyedondoka. Nae Herbert Luyinda, mjomba wa marehemu amesema mipango yote inaenda vizuri na na mwili unategemea kuwasili Uganda siku ya Jumapili ukitokea Afrika ya Kusini ambako ndiko mauti yalimkuta Ivan. Mazishi yanategemewa kuwa siku ya Jumanne.

No comments:

Post Top Ad

Powered by Blogger.