MCHUNGAJI NA WASAIDIZI WAKE WAHUKUMUMIA KIFUNGO CHA MIAKA 30 KWA KUUWA


Watuhumiwa wakiwa na Pastor Juan Rocha (aliyejiinamia)
Mchungaji mmoja na wasaidizi wake wanne wamehukumiwa kufungwa miaka 30, kwa kosa la kumchoma moto mpaka kumuua mwanamke mmoja kwa kisingizio cha kumuondoa mapepo. Mwanamke huyo Vilma Trujillo mwenye umri wa miaka 25 alifariki mwezi February, baada ya kufungwa mikono na miguu na kutupwa kwenye moto. Mkasa huu uliotokea huko Nicaragua, ulimfanya Jaji  Alfredo Silva atamke wazi kuwa mateso aliyoyapata Trujillo, hayafai kumpata binadamu yoyote mwingine. Pastor Juan Rocha mwenye umri wa miaka 23, na nduguze wa tumbo moja, Tomasa na Pedro Rocha, na wasaidizi Franklin Jarquin na Esneyda Orozco wote walipatikana na hatia ya mauaji. Mume wa marehemu Reynaldo Peralta Rodriguez alisema ‘Hawa wamemuua mke wangu, mama wa watoto wawili wadogo ntawaambia nini wakikua? Trujillo aliyekuwa mkazi wa kijiji El Cortezal, alifariki baada ya kulazwa wiki moja hospitalini alikokuwa anatibiwa baada ya kuungua asilimia 80 ya mwili wake kutokana na mkasa huo. Watuhumiwa hawakuonyesha dalili yoyote ya kushtuka baada ya hukumu kutolewa.

1 comment:

Post Top Ad

Powered by Blogger.