MGOMBEA URAIS AMBAE PICHA ZKE ZA UTUPU ZILISAMBAA MITANDAONI AMESEMA ATAENDELEA NA SAFARI YAKE YA KUELEKEA IKULU

Diane Shima Rwigara
Yule mdada wa Rwanda ambaye alisema lazima agombee urais wa Rwanda uchaguzi ujao, na wiki mbili zilizopita picha zake za utupu zikasambazwa kwenye mitandao, amerudi tena na nguvu mpya. Diane Shima Rwigara, amerudi tena hewani baada ya kupotea mara tu picha zake ziliposambaa na amesisitiza nia yake ya kugombea urais wa Rwanda kwenye uchaguzi mkuu mwezi wa nane iko palepale. Diane alichukua fomu ya kugombea urais kwenye ofisi za tume ya uchaguzi siku ya tarehe 10 May, akiwa kajiandikisha kama mgombea binafsi. Diane alizikataa picha zilizosambaa na kusema zimetengenezwa, picha hizi zilisambaa sana katika blogs za Nigeria na Kenya. Leo ndio kwa mara ya kwanza Diane ameanza kuonekana tena kwenye mitandao ya jamii, mwenyewe amesema alipotea kwa kuwa kuna watu waliteka account zake , na hata kuzifuta bila makubaliano yake. Diane Shima Rwigara ni binti wa mfanya biashara maarufu Assinapol Rwigara, aliyefariki katika ajali ya gari mwaka 2005 na Diane amekuwa akidai baba yake aliuwawa na ajali ilikuwa kisingizio tu.

No comments:

Post Top Ad

Powered by Blogger.