MJUE MWANAMKE MWAFRIKA ALIYEMWEZESHA RAIS MPYA WA UFARANSA KUSHINDA UCHAGUZI


Sibeth Ndiaye
GAZETI   la  Le Monde la huko Ufaransa, limeanza kuandika wasifu wa Sibeth Ndiaye, mama wa miaka 37, Mfaransa mzaliwa wa Senegal ambaye ndie mmoja wa washauri wakuu wa  Emmanuel Macron, Rais mpya wa Ufaransa. Na inasemekana ndie atakaekuwa Msemaji Mkuu wa Rais huyu mpya.
Ndiaye anaonekana ndie mmoja wa vinara wa mafanikio ya Macron. Kwa mujibu wa gazeti la Le Monde mama huyu, na mke wa Macron ndio wanawake waliokuwa muhimu zaidi katika kambi ya uchaguzi ya Rais Macron. Ndiaye ameonekana ni mtu muhimu sana katika filamu inayotayarishwa inayoongelea yaliyokuwa yanatokea wakati wa matayarisho ya kugombea urais. Katika filamu hiyo ukaribu wa Macron na huyu mama unaonekana wazi kwani wanaonekana wanataniana, wanacheka, Ndiaye anaonekana akimhamasisha asikate tamaa, na hata kumtayarishia ratiba mbalimbali za shughuli zake. Mama huyu ambaye amesuka nywele katika mtindo wa dread, na mara nyingi akiwa amevaa raba za bluu za Adidas, hakufanana kabisa na wanasiasa wa kawaida katika mfumo  wa  Ufaransa.  Ndiaye alikulia Dakar, mji mkuu wa Senegal, akiwa mtoto wa nne na wa mwisho, katika familia iliyopenda sana siasa. Wazazi wake wote walikuwa ni viongozi wa juu katika serikali ya Rais  Abdoulaye Wade.

No comments:

Post Top Ad

Powered by Blogger.