MKASA ULIOIKUTA TBC WAVIKUTA VYOMBO VYA HABARI VYA QATAR


UNAKUMBUKA  mkasa uliowapata watangazaji wa TBC wakalazimika kusimamishwa kazi baada ya kutangaza habari waliyoikuta kwenye mitandao kumbe ilikuwa si ya kweli? Basi mkasa kama huo umevikuta vyombo viwili vikubwa vya nchini Qatar. TV za Sky News Arabia na Al Arabiya  zimejikuta zikitangaza habari ambayo ilidaiwa ilisemwa na kiongozi wa Qatar. Emir  Sheikh Tamim bin Hamad Al Thani. Si tu habari hizi zilitangazwa lakini wananchi pia walikaribishwa kutoa maoni yao kuhusu matamko hayo ambapo Emir huyo alisemakana alisema kuwa anaunga mkono Iran, Hamas, Hezbollah na Israel, na pia kutoa tamko kuwa hadhani kama Rais wa Marekani Donald Trump atamaliza muda wake madarakani. Tatizo lilikuwa wadunguaji wa mitandao, ‘hackers’, walikuwa wameingia katika tovuti ya Quatar News Agency na kuweka taarifa hiyo ya uongo. (hacking of Qatar News Agency's website) .Waziri wa Mambo ya Nje wa Qatar akizungumzia hilo siku ya Jumatano huko Doha alisema, ‘Kwa kuwa kuna sheria za Kimataifa za makosa haya ya mtandaoni, waliofanya kosa hilo watasakwa na kushtakiwa ipasavyo. Lakini jambo la ajabu ni kuwa pamoja naserikali kuvitaarifu vyombo hivyo vya habari kuwa taarifa vinayotumia si ya kweli, vyombo hivyo viliendelea kutumia taarifa hiyo, jambo ambalo nalo limeleta mgogoro kuhusu ufanisi wa taaluma ya uandishi katika vyombo hivyo.

No comments:

Post Top Ad

Powered by Blogger.