MSANII MWIGIZAJI APIGWA RISASI NA MAJAMBAZI SOWETO


Msanii maarufu Mandla Hlatshwayo ambaye pia alikuwa anaigiza kwenye tamthiliya ya South Africa ya Generations usiku wa kuamkia leo 15 May 2017, ameuwawa na majambazi ndani ya baa moja huko Pimville Soweto. Mandla ambaye pia alikuwa DJ wa kituo cha redio cha  Jozi FM, alipigwa risasi kiasi cha saa tano usiku, baada ya majambazi wanne wenye silaha kuingia ndani ya baa hiyo na kuanza kuibia watu.  Msemaji wa polisi Captain Hitler Mngwenya alisema Mandla  na mwenzie mmoja walikuwa wakijaribu kuwasaidia waliokuwa wakiibiwa ndipo wakapigwa risasi na majambazi hao.
Waziri wa Sanaa na Utamaduni wa Afrika ya Kusini Nathi Mthethwa amesema kifo cha  msanii huyu ni cha kushtua na kusikitisha. Mandla Hlatshwayo alikuwa akiigiza kama  Siphiwe Phosa kuanzia mwaka 1999 mpaka  2006 katika tamthiliya ya Generations.

No comments:

Post Top Ad

Powered by Blogger.