MUUAJI MANCHESTER-BABA WA MUUAJI, NA MWANAE MWINGINE WAKAMATWA


BABA  mzazi na mdogo wake wa Salman Abedi, kijana aliyejilipua na kuuwa watu wengi nje ya ukumbi wa muziki huko Manchester wametiwa nguvuni nchini Libya. Baba mtu Ramadhan Abeid na mwanawe  Hashem, wako chini ya ulinzi kwa tuhuma za kuwa na uhusiano na ISIS. Kaka mkubwa wa aliyejilipua alikamatwa jana Jumanne huko
Chorlton, kusini mwa Manchester. Wakati huohuo Waziri wa Mambo ya Ndani wa Uingereza ameijia juu Marekani kwa kutangaza jina la mtuhumiwa mapema kabla polisi wa Uingereza hawajamtangaza, jambo ambalo linaweza kuharibu upelelezi.  Vyombo vya habari vya  CBS and NBC  ndivyo vilivyokuwa vya kwanza kumtaja Salman Abedi kama ndie aliyejilipua na kuuwa watu, vyombo vya usalama vya Uingereza vilikuwa bado vimeficha jina hilo ili kuweza kupeleleza kwa ufanisi zaidi.

No comments:

Post Top Ad

Powered by Blogger.