MUGABE HALALI ANAPUMZISHA MACHO TU
Serikali ya Zimbabwe imesema Rais wake kuonekana amelala kwenye mikutano ni kutokana na yeye kufunga macho kuyapumzisha na pia kukwepa mwanga mkali, kwani mwanga umekuwa unamsumbua macho. Kifupi tu ni kuwa picha zote zinazoonyesha amelala usingizi, si usingizi ni kufumba mamcho tu kuyapumzisha. Hayo yamesemwa na George Charamba alipokuwa anaongea na gazeti la serikali la nchi hiyo  Herald. Mugabe ambaye sasa ana miaka 93, amekuwa akipigwa picha akiwa katika ‘pozi’ la kulala mara nyingi na kuchochea moto tuhuma za matatizo ya afya yake. Hivi karibuni Rais huyo alienda Singapore kutibiwa macho. Katika mkutano wa karibuni wa  World Economic Forum uliofanyika Afrika ya Kusini mapema mwezi huu, kwa mara nyingine Rais huyu alipigwa picha akiwa katika pozi ya kuwa usingizini.  Kwenye mkutano huyo Mugabe aliisifu nchi yake kuwa ni moja ya nchi zenye maendeleo makubwa Africa. Bwana Charamba alilinganisha tatizo la macho ya Mugabe na lile la macho ya Nelson  Mandela aliyepata matatizo ya macho kutokana na kufanya kazi kwa miaka mingi katika machimbo ya chaki wakati akiwa mfungwa wa Kisiwa cha Robben.

No comments:

Post Top Ad

Powered by Blogger.