MWANAHARAKATI WA MAPENZI YA JINSIA MOJA ASWEKWA RUMANDE


Kasha Jacqueline Nabagesera
Kasha Jacqueline Nabagesera raia wa Uganda anaejulikana kwa harakati zake za kutetea mapenzi ya jinsia moja, amewekwa chini ya ulinzi wa polisi alipofika tu uwanja wa ndege wa Kigali huko Rwanda. Anatuhumiwa kwa ulevi na kufanya fujo. Kwa maelezo ya ukurasa wake wa tweeter, Kasha alienda Kigali kukutana na watengeneza filamu wa Kimarekani. Askari wa Rwanda wamesema amekamatwa na hatua stahiki zitafuatwa kutokana na kosa lake. Kama ilivyo kwenye nchi nyingi za Afrika, mapenzi ya jinsia moja hayaruhusiwi nchini Uganda

No comments:

Post Top Ad

Powered by Blogger.