MWANAMUZIKI AJINYONGA MUDA MFUPI BAADA YA KUMALIZA ONYESHO


Mwanamuziki muimbaji  Chris Cornell amejinyonga. Cornell aliyekuwa na umri wa miaka 52, alikutwa amekufa baada ya onyesho alilofanya na bendi yake ya Soundgarden, katika jiji la Detroit juzi Jumatano. Familia yake wamesema wanataka kumzika bila kuwa na watu wengi. Kwa kadri ya maelezo yaliyotolewa ndugu yake mmoja alikuwa anamtafuta akamkuta sakafuni bafuni, walipomkimbiza hospitali alikuwa amekwisha kufa. Cornell alizaliwa 20 July, 1964.
Amekwisha toa album 4, ya mwisho ikiwa inaitwa Higher Truth aliyoitoa 2015. Wimbo wake uliomletea fedha nyingi na umaarufu ulikuwa ni You Know My Name, ambao ulitumika kama ‘theme song’ ya filamu ya Casino Royale, ya James Bond. Siku ya Jumatano ali tweet picha za bendi yake ikiwa jukwaani siku hiyo, cha ajabu ni kuwa muda mfupi baadae alijinyonga.

No comments:

Post Top Ad

Powered by Blogger.